Thursday, May 8, 2014
WANANCHI WATAKIWA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA MKOANI NJOMBE
Jamii Mkoani NJombe Imeshauriwa Kushirikiana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Pamoja na Serikali Katika Kupinga Vitendo Vya Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia Vinavyofanywa na Baadhi wa Watu Katika Mazingira Yanayowazunguka.
Rai Hiyo Imetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Njombe Abraham Kaaya Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi wa Warsha ya Siku Nne Inayotolewa na Shirika Lisilo la Kiserikali la IDYC Inayolenga Kupinga Ukatili wa
Kijinsia Katika Jamii.
Akizungumza Wakati wa Kufungua Warsha Hiyo Bwana Kaaya Amewataka Washiriki Kuyatumia Vizuri Mafunzo Wanayoyapata Ili Kusaidia Kutokomeza Vitendo Vya Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia Katika Jamii Inayowazunguka , Kama Anayoeleza.
Awali Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa IDYC John Nkoma Ameelezea Baadhi ya Shughuli Zinazofanywa na Shirika Hilo Ikiwemo Kuwasaidia Watoto Yatima Katika Masomo, Kuziwesha Familia Kiuchumi, Kuanzisha Mradi wa Afya Kwa Kutoa Elimu Kuhusu Masuala ya Ukimwi Pamoja na Madhara ya Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Akielezea Lengo Kuu la Warsha Hiyo Mwezeshaji Abou Makalabo Amesema ni Kuwa Jengea Uwezo Wadau Mbalimbali Ili Waweze Kuwahusisha Wanaume Katika Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Huku Baadhi ya Matarajio Yakiwa ni Kuwaondoa Wanawake na Wasichana Kuwaondoa Katika Mazingira ya Ukatili wa Kijinsia na Washiriki wa Warsha Hiyo Kuonyesha Mabadiliko Chanya Katika Jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment