Friday, May 9, 2014
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AHIMIZA TOHARA KWA WANAUME
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIWASILI KATIKA UWANJA WA MKUTANO WELELA
HAWA NI WANANCHI WA KIJIJI CHA WELELA WAKISIKILIZA HOTUBA YA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIONGEA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA WELELA KATA YA MTWANGO WILAYANI NJOMBE
SHUKRANI ZIKITOLEWA NA WANANCHI KWA KUFIKA KATIKA KIJIJI HICHO KWA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE KWANI HAKUNA VIONGOZI WENGINE WA WILAYA WENYE MOYO WA KUWAFIKIA WANANCHI WAKITOA MWALIKO WOWOTE.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sarah Dumba leo amefanya ziara ya siku moja kwa kutembelea vijiji vya matiganjora,Welela na Ibumila ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuhamasisha wananchi kushiriki katika kampeni ya Tohara kwa wanaume ambayo itasaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Akizunguzungumza na wananchi akiwa katika ziara hiyo Bi. Sarah Dumba amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuepukana na Imani potofu kuhusiana na Tohara kwa wanaume ambapo kauli hiyo imekuja kutokana na baadhi kuamini tendo hilo linahusiana na imani ya dini ya kiislamu.
Bi. Dumba amesema kuwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa maambukizi ya UKIMWI ni pamoja na kuwepo kwa ulevi uliokithiri miongoni mwa wanajamii,Mila potofu za kurithi wajane, kuwa na wake zaidi ya mmoja na ngono zembe pamoja na kutofanya tohara kwa wanaume jambo ambalo linasababisha ongezeko la ugonjwa huo .
Akisoma Taarifa fupi juu ya Tohara kwa wanaume kaimu Mratibu wa kudhibiti na Kupambana na UKIMWI Wilaya ya Njombe bwana Nicko Mandele amesema kuwa viongozi wa vijiji na kata wanatakiwa kuwahamasisha wanaume kufika kufanyiwa tohara katika vituo vinavyotoa huduma hiyo ili kupunguza Maambukizi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa ya Saratani ya shingo ya Kizazi na kutungwa kwa mimba nje ya mfuko wa uzazi kwa wanawake.
Akisoma taarifa fupi ya kijiji cha Welela afisa mtendaji wa kijiji hicho bwana Thomas Mwinami amesema wananchi wa kijiji hicho wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa zahanati ya kijiji,miundombinu ya maji,upungufu wa nyumba za walimu na madarasa pamoja na miundombinu ya barabara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment