Friday, May 9, 2014
MKUU WA MKOA WA NJOMBE LEO AMEZINDUA CHANJO CHA PILI KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIEZI 18.
MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi leo amezindua chanjo ya pili ya kuzuia Ugonjwa wa Surua kwa watoto chini ya umri wa miezi 18 mkoani Njombe kufuatia Chanjo ya awali kushindwa kuzuia ugonjwa huo kwa asilimia 100 ambapo Zaidi ya watoto elfu 18 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo.
Akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi huo Keptain Mstaafu Msangi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao kupatiwa chanjo hiyo huku akiitaka Idara ya Afya kuhakikisha ifikapo mwezi July mwaka huu wawe wamekwisha kutoa taarifa ya Utekelezaji wa zoezi hilo.
Aidha Keptain Msangi ameitaka idara ya afya kushirikiana na vyombo vya habari mkoani Hapa ikiwemo UPLANDS FM RADIO kuhakikisha wanatoa taarifa juu ya ugonjwa wa DENGE ambao umeanza kuwa tishio hapa nchini baada ya kuibuka mkoani Dar Es Salaam na kuiwasilisha taarifa hiyo katika kikao cha RCC mwezi huu.
Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo ya Surua Mkoa wa Njombe b. Linda Chatila amesema kuwa jumla ya vituo mia 201 kati ya 238 vinatarajia kutoa Chanjo hiyo ambayo hutolewa kwa Watoto wenye umri wa miezi 18 ambapo lengo la Chanjo ya pili ya Surua ni kukabiliana na Ugonjwa huo kwa asilimia 99 na kwamba mtoto hukingwa kwa asilimia 89 .6 wakati anapatiwa chanjo ya kwanza akiwa na miezi 9.
Aidha Mratibu huyo Bi.Chatila amesemsa kuwa uzinduzi huo mpya wa chanzo ya surua awamu ya pili umeanza rasmi Mei Mosi mwaka huu baada ya kufanyika kwa uzinduzi wake kitaifa Mkoani Kilimanjaro na mke wa Rais mama Salma Kikwete.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment