MAHABUSU NA WANANCHI MAKETE WALIA KUKOSEKANA KWA HAKIMU
MAHABUSU NA WANANCHI MAKETE WALIA KUKOSEKANA KWA HAKIMU,Na hivyo kuahirishwa Kesi Mara kwa mara.
Wananchi wakisubiri kesi zao zianze.
Na Edwin Moshi wa Globu ya Jamii, Makete.
Watuhumiwa
na walalamikaji mbalimbali wenye kesi zao katika mahakama ya wilaya ya
Makete mkoani Njombe wameendelea kuonja tena machungu ya kuahirishiwa
kesi zao leo Ijumaa Mei 09, kwa kile kilichoelezwa kuwa hakimu kushindwa
kufika
Wakisikika
wakiongea mahakamani hapo wakiwa katika makundi makundi, wamesema
hawakatai wao kuahirishiwa kesi zao ila zinapoahirishwa mara kwa mara
kwa muda mrefu inawaumiza wananchi ukizingatia wengi wao wanatumia fedha
nyingi ili kuweza kuhudhuria mahakamani
Wakisikiliza taarifa ya kuahirishiwa kesi zao.
“Hakimu
wa wilaya sisi hatuna, hebu fikiria mara ya mwisho hakimu amefika hapa
mwezi wa Februari akasikiliza kesi zetu vizuri tu, lakini tangu hapo
tumekuwa tukiahirishiwa tu kesi kila tukija, na sababu tunaambiwa hakimu
ametingwa na majukumu mengine, sasa jamani hii kero ni hadi lini”
alisikika mmoja wa waliofika mahakamani hapo akizungumza
Licha
ya kuongezeka kwa kesi na huduma mbalimbali za kimahakama katika
mahakama ya wilaya ya Makete, bado wilaya hiyo imeendelea kusota kwa
kukosa hakimu wa mahakama hiyo hivyo hakimu kutoka mahakama ya Njombe
hulazimika kuja kuendesha kesi katika mahakama ya wilaya ya Makete na
mahakama yake ya Njombe
Kutokana
na jiografia ya Makete, mtu mwenye kesi katika mahakama ya wilaya kama
yupo nje ya Makete mjini hulazimika kutumia gharama kubwa za kusafiri
hadi kufika mahakamani kutokana na uhaba wa magari ya usafiri
“Kwa
mfano sisi tuliahirishiwa kesi juzi tarehe 30 Aprili tukaambiwa tuje
leo, bado na leo ni kama yale yale tu, mimi naiomba serikali itupe
hakimu wetu kwa sababu huyu hakimu anatoka Njombe na huko ana kazi za
kimahakama yake pia sasa akitingwa si rahisi kuja huku” amesema
mwananchi mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake
Akitoa
taarifa ya kuahirishwa kesi hizo hii leo Mkuu wa polisi wilaya ya
Makete (OCD) Alfred Kasonde amewapa pole wananchi hao wenye kesi
mahakamani hapo na kusema anawaomba wawe wavumilivu, na kesi zao
zimeahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu
Wakiondoka baada ya kesi zao kuahirishwa.
“Jamani
naimani mmenisikia jinsi nivyokuwa nazungumza nao kwenye simu,
nimewaeleza hali halisi lakini ndio hivyo tena, mimi nawaomba muwe
wavumilivu yatakwisha tu, kila kitu kitakwenda sawa, naombeni mje kwa
ajili ya kesi zenu tarehe 23 mwezi huu, poleni sana” amesema Kasonde
No comments:
Post a Comment