Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, May 8, 2014

WENYEVITI NA MAMENEJA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU TATU




Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Akiba  na Mikopo Mjini Njombe wameshauriwa kutatua migogoro na changamoto  zinazovikabili vyama hivyo  ambapo pamoja na mambo mengine wametakiwa kufuatilia mikopo kwa umakini kwa wateja wake ili kuwafanya wananchi waweze kuviamini vyama hivyo na kuweza kujiunga.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu mwanasheria wa halmashauri ya mji wa Njombe  bwana Bahati Kikoti wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wenyeviti na Mameneja wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo yaliolenga kuwaongezea uelewa viongozi wa SACCOS na kuwataka kuyatumia vizuri na kwa manufaa ya vyama vyao.

Katika Hotuba yake kwa washiriki wa Mafunzo ya viongozi wa SACCOS Bwana Kikoti amesema kuwepo kwa udhaifu  wa usimamizi  kwa viongozi wa vyama hivyo  umesababisha baadhi ya SACCOS kukosa wateja na kwamba wanachama wanatakiwa kurejesha mikopo kwa wakati ili kujengewa uaminifu na taasisi zinazowakopesha.

Aidha bwana Kikoti amesema kuwa maafisa Ushirika wa halmashauri wanatakiwa kuwafikia wanachama wa vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo SACCOS   vilivyopo katika Halmashauri ili kutoa elimu  juu ya uendeshaji pamoja na namna ya kutatua matatizo yanayovikabili vyama hivyo.

Mwenyekiti  wa Mafunzo hayo ambae  ni kaimu mwenyekiti wa Chama cha ushirika cha Akiba na Mikopo cha wafanyabiashara  Njombe Mjini bwana Joseph Mwaluwanda ameahidi  kuyafanyia kazi  na kwamba yaliozungumzwa na Mgeni rasmi kwa wanachama hao ikiwemo   matatizo yanayozikabili SACCOS,kutunza nidhamu,kutoa taarifa za hesabu za mapato na matumizi pamoja na kudumisha dhana ya utawala bora kuwa kila chama kikayafanyie kazi.

Wakizungumza mara baada ya kufunga mafunzo hayo washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanaamini mabadiliko yatakuwepo  kwenye vyama vyao  huku wakiomba maafisa ushirika kuwafikia kwenye vyama vya ushirika kutoa elimu hiyo kwa wanachama wote ili nao wanufaike kama walivyonufaika viongozi hao.

Jumla ya viongozi 28 walioshiriki  mafunzo  hayo wa kutoka vyama 14 vya halmashauri ya mji wa Njombe wamepokea vyeti vya ushiriki mafunzo hayo ambayo yametolewa kwa siku tatu na Maafisa ushirika wa halmashauri ya mji wa Njombe,CRDB, NSSF  na maafisa kutoka Idara ya kazi mjini Njombe.



 

No comments:

Post a Comment