Na Steven Ngole Njombe
Wanafunzi Watatu wa Shule ya Msingi Ibumi Wamefariki dunia Baada ya Kujaribu Kuogelea katika Dimbwi la maji Wilayani Ludewa.
Kufuatia Tukio Hilo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Vifo Vya Wanafunzi Watatu wa Shule ya Msingi Ibumi Wilayani Ludewa Baada ya Kujaribu Kuogelea Kwenye Dimbwi la Maji Wakati wa Kitoka Shuleni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Aprili Tatu Mwaka Huu Majira ya Saa Kumi Jioni Ambapo Watoto Hao Walipita Kwenye Dimbwi Hilo Lililokuwa Likitumika Kwa Ajili ya Kufyatulia Tofali na Kujaribu Kuongelea.
SACP Ngonyani Amewataja Watoto Waliofariki Kuwa ni Kasbeth Kasbeth Miaka 6 Ambaye Alikuwa Hajaanza Shule,Noeli Msemwa Miaka 8 Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza na James Haule Miaka 9 Mwanafunzi wa Drasa la Pili Wote Walikuwa Wanafunzi Katika Shule ya Msingi Ibumi Wilayani Ludewa.
Akielezea Tukio Hilo Kamanda Ngonyani Amesema Katika Tukio Hilo Walikuwa Watoto Wanne Ambaye Mmoja Kati Yao
Alikimbia Kutoa Taarifa Baada ya Kuona Wenzake Wanazidiwa na Maji Alikimbia Kutoa Taarifa.
Katika Hatua Nyingine Kamanda Ngonyani Ametoa Wito Kwa Wananchi Kuchukua Tahadhari Zaidi Katika Kipindi Hiki Ambacho Mvua Zinaendelea Kunyesha na Kuwataka Wananchi Kufukia Mashimo Yote Ambayo Yanahifadhi Maji Ili Kuepusha Vifo Viunavyoweza Kuepukika.
Matukio ya Vifo Vitokanavyo na Ajali ya Maji Yamekuwa Yakiendelea Kutokea Katika Mikoa Maeneo Mbalimbali Mkoani Njombe Ambapo Wahanga Wakubwa wa Matukio Haya ni Watoto.
No comments:
Post a Comment