Saturday, April 5, 2014
FEMA HIP WATARAJI KUFANYA TAMASHA LEO VIJANA WAHUSIKA ZAIDI
mkurugenzi wa Shirika la Fema HIP Bi.Amabilis Batamula akibadilishana mawazo mara baada ya semina hiyo leo na mkurugenzi wa mtandao huu Ambaye pia ni Katibu wa Shirika la NJOMBE YOUTH DEVELOPMENT ARGANIZATION[NJOYODEO]
Katibu wa NJOYODEO Bwana Gabriel Kilamlya akipokea cheti cha kufuzu ushiriki wa mafunzo ya Fema Hip leo katika ukumbi wa Milimani Motel
Na Festo James Njombe
Vijana wanaomaliza katika vyuo mbalimbali nchini wameshauriwa kujitolea katika shughuli za kijamii ili kuongoza ujuzi utakaowarahisishia kupata ajira katika fani walizozisomea.
Akiongea Katika semina ya siku moja ya shirika la femina kwa asasi zisizo za kiserikali mkoani njombe ambao hutumia na kusambaza majarida yao Afisa wa shughuli za nje Bi Costancia Mgimwa amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakikosa fursa za ajira kutokana na kutokuwa na uzoefu katika kazi wanazozombea ajira hivyo ni vema kujenga uzoefu kwa kujitolea.
Katika Hatua Nyingine Bi Mgimwa Amewataka Asasi washiriki katika Semina Hiyo kuwajengea Uwezo wa
kunufaika Kiuchumi kwa Kutokana na Rasilimali Zilizopo Nchini Yakiwemo Madini Pamoja na Ufanisi katika Kazi.
Akiongea na www.gabrielkilamlya.blogspot.com hii leo mkurugenzi wa Shirika la Fema HIP Bi.Amabilis Batamula amesema kuwa lengo la Kufanya semina hiyo nikutaka kujua ni namna gani bidhaa zao zinatumika ambapo amezitaka Asasi hiyo Kuunda hoja katika majarida hayo pamoja na kuzijadili ili kuongeza uelewa kwa vijana ambao ni walengwa wa shirika hilo.
Aidha Bi Batamula Amesema Kuwa Mkoa wa njombe ni mkoa ambao unaongoza kwa kupata nakala nyingi za kuliko mkoa mwingine nchini lakini majarida hayo yamekuwa hayatoshi na kuongeza kuwa wapo mkoani Njombe kwa siku kumi na miongoni mwa vitu wanavyotarajia kufanya ni pamoja na tamasha, semina, na Kuongea na Asasi Pamoja na Wananchi Kuhusu masuala ya Vijana na Maendeleo.
Kwa Upande wao Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka katika mashirika ya Vijana Mkoani Njombe Wamesema wasema kuwa licha FEMA Kuendelea kutoa elimu lakini wanahitajika kuongeza majarida kwa ajili ya kuwasambazia vijana
Miongoni mwa changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili ni pamoja na upatikanaji wa fedha toka kwa wafadhili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment