Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, April 5, 2014

CHUNGU CHA AJABU CHAIBUKA JUU YA KABURI KIKIFOKA DAMU -IRINGA


Chungu  cha ajabu  kilichokutwa juu ya kaburi  katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa  leo kikiwa  kinafoka  damu
Wananchi  wakishuhudia chungu  hicho cha ajabu  kushoto  karibu na jembe
Hapa  ndipo  chungu hicho  kilipoibukia
Baba wa mtoto Agnes Mlawa akichimbua chungu  hicho
baba  wa mtoto huyo kulia akisaidiwa na msamalia  mwema  kufungua chungu hicho ili kuona ndani
Hivi ndivyo  vilivyokuwemo ndani na damu ,maini na kichwa cha ndege
Hapa msamaria  mwema  akionyesha vitu  vilivyopo ndani
Mzee Mlawa  akiwasha kiberiti kwa ajili ya kuteketeza  ushirikiana huo
Tunguli ikiteketezwa  kwa moto
Wananchi na mzee Mlawa  kulia  wakitazama tunguli hilo  likiteketea kwa moto
Mwisho wa ushirikina hapa
MAUZA  uza matupu  kaburi  la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi  wa Ilala  katika Manispaa ya  Iringa aliyezikwa mwaka  jana na leo baba  wa  mtoto  huyo kakuta chungu cha ajabu chenye damu,maini na kichwa cha ndege kimechimbiwa  kaburini.

Tukio  hilo la aina  yake  limetokea leo majira ya saa 2 asubuhi  katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati  baba mzazi wa mtoto  huyo Bw. Mlawa  wakati  akichembua kaburi  hilo na mara  baada ya  kumaliza  ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu  cha ajabu  kuibuga juu ya kaburi  hilo .

" mimi hapa leo  nilikuja  kusembua  kaburi la mwanangu  ila  baada ya  kumaliza  ghafla  nilikuta kama damu  zinaruka juu  kutoka kaburini na baada ya  kuchunguza  ndipo nilipoona  chungu hicho kikiibuka huu ya kaburi "

Alisema  kuwa chungu  hicho kilikuwa  kimefungukwa na kitambaa cheusi juu ambacho  kimelowa  dawa  na kufungwa kamba ya  nguo ya  kijani  na kutokana na  tukio hilo la ajabu alilazimika  kuacha jembe  juu ya kaburi na kukimbia  kuita  watu  wanaopita barabarani  ili  kuomba msaada zaidi.

Mzazi   huyo anadai kuwa  mazingira ya kifo cha mtoto  wake  yalikuwa ni ya kushangaza  baada ya  kuugua kwa  muda wa  siku  nne pekee na kufariki  dunia .

Hata  hivyo  alisema  kwa  kuwa kwa upande  wake haamini mambo ya kishirikiana  hakuona  sababu  ya  kumwita  mganga  wa  kienyeji kwa ajili ya  kushughulikia  kuchoma chungu  hicho na badala  yake  kuamua  kuifanya kazi  hiyo mwenyewe hasa  akiamini nguvu ya Mungu  zaidi.

" Napenda  kuwashukuru  wananchi  waliofika  hapa kwa kunitia  nguvu na  pia kuwashukuru madereva  boda  boda  akiwemo kijana  Ahmed kwa  kujitolea  mafuta  ya Petrol kwa  ajili ya kukichoma chungu  hiki "

Mbali ya  mzazi   huyo  kujitolea  kuchuma chungu  hicho na kuteketeza  vitu vilivyo kuwemo ndani wananchi  waliofika  kushuhudia  tukio  hilo  walilazimika  kutimua  mbio  kuhofu zoezi hilo la uchomaji wa  tunguli  hizo.

No comments:

Post a Comment