WANANCHI
wenye hasira kali wakazi wa mtaa wa Mtwivila D katika Manispaa ya
Iringa wamemuua mtuhumiwa mwingine wa ujambazi aliyetambulika kwa jina
la Ayubu Mhema (31) msukuma mkokoteni mkazi wa Wangama mkoani Njombe
kwa tuhuma za wizi wa mali za wananchi wa eneo hilo.
Tukio
hilo lilitokea leo majira ya saa 3 asubuhi baada ya mtuhumiwa
huyo kukamatwa akiwa na nguo zilizojaa ngunia moja ambazo aliziiba
katika nyumba ya mkazi mmoja wa eneo hilo baada ya kuvunja
mlango
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi pasipo kutaja majina yao wananchi
hao walisema kuwa kumekuwepo na matukio endelevu ya wizi katika
eneo hilo na mbali ya wezi hao kukamatwa na kufikishwa polisi ila
bado wamekuwa wakiachiwa huru jambo ambalo limeongeza wimbi la wizi
katika eneo hilo.
Hata
hivyo walisema mtuhumiwa huyo Mhema amepatwa kukamatwa eneo hilo
zaidi ya mara nne akiwa na wenzake ila mbali ya kupewa kichapo
bado amekuwa akirudia kuiba .
Mbali
ya kulalamikia matukio hayo ya wizi yanayoendelea katika eneo
hilo bado waliwatuhumu viongozi wa serikali ya mtaa kwa kushindwa
kuitisha mkutano wa dharula kwa ajili ya wananchi kupiga kura ya
siri kwa lengo la kuwataja watu ambao wamekuwa wakijihusisha na
mtandao wa wizi na wale wanaofunga mtandao huo ambao baadhi yao
wanadaiwa ni viongozi wa mtaa huo.
"
Tumekuwa tukiomba kufanyika kwa mkutano na kila wiki mtendaji na
mwenyekiti wamekuwa wakisogeza mbele mkutano huo huku wananchi
tukiendelea kunyanyasika na mtandao huo wa wezi ....ila tunasubiri
kwa mara nyingine mkutano wa April 27 kama walivyotangaza na iwapo
watashindwa tutapambana na viongozi hawa kwa kumkataa mtendaji wa mtaa
na kata pamoja na wajumbe wake wote "
Kwani
walisema katika mkutano wa mwisho uliofanyika mwezi uliopita mbele
ya diwani wa kata ya Mtwivila Vitus Mushi wananchi kwa kauli moja
waliomba mkutano huo ila viongozi hao wamekuwa wakimpuuza hadi
diwani wao kwa kushindwa kusikiliza maombi ya wananchi .
Pia
walisema orodha kamli ya majina ya mtandao huo wa wezi ilitajwa
na mtuhumiwa huyo Mhema kabla ya kufariki ambapo mtandao huo upo
stendi ya Mlandege ,stendi kuu , Ilala kwa Mlyuka pamoja na Kihesa
ambako ndiko yupo mmiliki wa mtandao huo ambapo majina yao
yamehifadhiwa .
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia polisi wakifika eneo hilo wakiwa na
mabomu ya machozi kwa ajili ya kumuokoa mtuhumiwa huyo na kumchukua
kumkimbiza Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kabla ya kufariki
dunia njiani .
Ndani
ya wiki hii moja wananchi hao wa mtaa wa Mtwivila D wamewatesa
hadi kufa watu wawili kwa tuhuma za wizi ambapo jeshi la polisi
limewaonya wananchi hao kuacha tabia ya kujichukulia sheria
mkononi dhidi ya watuhumiwa wa wizi na kuwa kufanya hivyo ni kosa
na ni kinyume na haki za binadamu. |
No comments:
Post a Comment