Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, April 20, 2014

MWENYEKITI WA BODI LUPEMBE SEKONDARI AKANUSHA TUHUMA ZA KUUZWA KWA MSITU WA SHULE

 MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU AKITEMBELEA MAZINGIRA YA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE
 
 HUYU NI MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE BWANA CLEMENCE MALEKELA






MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKIWA KATIKA OFISI YA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE AKIHOJI MASWALI MBALIMBALI KWA MKUU WA SHULE HIYO NA VIONGOZI WA KATA NA HALMASHAURI KWA UJUMLA
HII NI SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE






MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKIKAGUA MIRADI YA SHULE INAYOTEKELEZWA IKIWEMO NYUMBA,MAABARA NA VYOO


BAADHI YA WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE WAKIHOJI MASWALI JUU YA MAKATO YA MSHAHARA WAO
WALIMU WATOA HISIA ZAO NA MALALAMIKO MBALIMBALI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAUL MALALA AKIJIBU MASWALI YA WALIMU
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIJIBIA SWALA LA KUUZWA KWA MSTU WA MITI
AFISA TAARAFA LUPEMBE BALTALTAZAR MVEYANGE






AKIWA KATIKA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE MKUU WA MKOA HUYO AKIWA NJIANI ALISHUHUDIA CHAI IKIWA BADO HAIJAPELEKWA KIWANDANI KWA KUKOSA USAFIRI KUTOKANA NA KUHARIBIKA KWA BARABARA


Siku chache baada ya Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi kuagiza  kufukuzwa kwa mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Lupembe kutokana na kutuhumiwa kuhusika na matumizi mabaya ya msitu wa shule hiyo mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Lupembe bwana Clemence Malekela amekanusha tuhuma zinazoikabili bodi hiyo.

Akizungumza na Uplands fm Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Lupembe bwana Clemence Malekela amesema tuhuma zinazoikabili bodi ya shule hiyo kuwa siyo za kweli kwa madai  msitu huo uliuzwa kwa maamuzi ya viongozi wa ngazi ya kata na taarafa pamoja na Mkuu wa shule hiyo kwa malengo ya kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu ya shule hiyo.

Bwana Malekela amesema  hatua ya viongozi wa taarafa,kata na bodi ya shule hiyo  kuuza miti ya msitu wa shule hiyo  Ilikuja kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya shule ikiwemo umeme,kukarabati  Na kujenga madarasa,kupeleka miundombinu ya maji,kukarabati nyumba 11 za walimu , mabweni na matumizi mengine ambapo jumla ya miti elfu moja mia  4 na 74 iliuzwa na kuacha miti mia saba 84 ambayo ilitoa mapato ya shilingi milioni 85 na laki 4 fedha ambayo ilipelekwa kwenye akaunti ya shule.

Amesema kuwa madai ya walimu ya kwamba malengo ya shule kupanda miti hiyo ilikuwa kupeleka miundombinu ya maji ni mtazamo wa walimu hao na kwamba mawazo hayo yalizungumzwa kinyume na taratibu za vikao vya bodi huku akisema vikao vya bodi huwakilishwa na mwalimu  mkuu  huku akisema   anahitaji apewe maandishi ya kusimamishwa kwa kuwa aliteuliwa kwa maandishi.

Bwana Malekela amesema kuwa tume ambayo mkuu wa Mkoa ameagiza ifike kuchunguza malalamiko hayo bodi hiyo ipo tayari kuyajibu kutokana na kila kitu kuwa wazi na kusema kuwa  jambo hilo bodi haijatendewa haki na kwamba imedhalilishwa huku ikishangazwa kuona  viongozi wa kata na taarafa kushindwa kutolea maelezo  malalamiko hayo kwa kuwa suala hilo lilikuwa wazi kwa wote.

Amesema kuwa fedha hiyo shilingi milioni 85 na laki 4 imekwisha tumika kwa kujenga vyumba vinne vya madarasa vilivyogharimu takribani mili0ni hamsini na nne,laini za nguzo za umeme zimegharimu milioni saba,nyumba za walimu 11 zimegharimu milioni sita  na nusu na nyingine  zimetumika kuboresha miundombinu mbalimbali ya shule hiyo.

Kwa upande wao viongozi wa taarafa na kata ya Lupembe akiwemo afisa taarafa ya Lupembe Baltazary Mveyange na diwani wa kata hiyo bi.Twilumba Wapalila wamekili kushiriki maamuzi ya kuuza miti ya msitu wa shule hiyo na kupanga matumizi yake huku wakisema matumizi ya fedha hizo yalivyofanyika mkuu wa shule aliyekuwepo mwaka 2011 wakati msitu huo ukiuzwa  ndiye aliyekuwa anafahamu zaidi.

Akiwa kwenye ziara ya Siku tatu ya kukagua miradi inayotekelezwa wilayani Njombe  mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi aliagiza kusimamishwa kwa mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Lupembe na wajumbe wake na kuahidi kupeleka wakaguzi na Tume ya kupambana na Rushwa Takukuru ili kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.


Mkuu wa Wilaya ya Njombe bi.Sarah Dumba akiwa kwenye ziara hiyo amesema kuwa utaratibu wa kuuzwa kwa msitu wa shule hiyo alifanikiwa kupewa taarifa kwamba kuna msitu unauzwa pasipo utaratibu na kumuagiza mkurugenzi  aliyekuwepo wakati huo Mohamed Mkupete ili kuingilia kati tatizo hilo ambapo ahadi ilikuwa maji yatapelekwa,nyumba za walimu zitakarabatiwa huku akisema ukarabati haukufanyika na kama ulifanyika haukukidhi viwango vyake.

Siku chache Wakizungumza mbele ya mkuu wa Mkoa wa Njombe walimu wa shule ya sekondari Lupembe pamoja na kulalamikia kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo za ukosefu wa miundombinu ya maji,uchakavu wa nyumba za walimu pamoja na kuwepo kwa makato ya mishahara ya walimu hao pia wamelalamikia kuishi katika mazingira magumu jambo lililosababisha wanafunzi kutokuwa na ufauru mzuri.

Aidha walimu hao Wamesema kuwa moja ya lengo la kuhamasika kupanda miti hiyo ilikuwa ni kuja kusogeza miundombinu ya maji na kujenga nyumba za walimu ambapo wameshangazwa kuona bodi ya shule imeingia na kuuza msitu huo pasipo wao kushirikishwa huku wakiendelea kuishi katika mazingira magumu kwa kufuata maji mtoni ambako wanatembea umbali wa takribani kilomita tatu jambo linalosababisha wanafunzi kukosa muda wa kujisomea.

No comments:

Post a Comment