MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKIKEMEA TABIA YA USHOGA,UKAHABA NA MAVAZI YASIYOSTAHILI KATIKA JAMII
AKINA DADA WAKILEO WADAIO HUU NI MTINDO WA KISASA WENGINE NI WAKE ZA WATU WENGINE WANATARAJIA KUPATA WACHUMBA HAPA KWELI
WALIMWENGU HILI NI VAZI LA HESHIMA KWA MWANAMKE KATIKA JAMII KIZAZI CHA SASA CHA ELEKEA WAPI
Mkuu wa Wilaya ya Njombe bi.Sarah Dumba ameziagiza halmashauri za Wilaya ya Njombe kutunga sheria ndogondogo zitakazo dhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria wafanyakazi wote wa biashara za vileo hususani wauzaji wa bar kutokana na kukiuka maadili ya jamii kwa kuvaa mavazi ya kubana yanayochora maumbile kinyume na sheria za nchi.
Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya bi.Dumba imetokana na kuwepo kwa wafanyakazi wa pombe za vileo yaani bar kuvaa suruali za kubana na kuchora maumbile yao pamoja na vijana wa kiume kuvaa suruali chini ya makalio jambo ambalo limechangia ukiukaji wa maadili ya wanafunzi wa shule za msingi na watoto wa nyumbani kutokana na kuiga tabia hiyo.
Katika hatua nyingine Bi.Dumba amekemea vikali suala la ndoa za jinsia moja pamoja na ukahaba na kuwataka wananchi kutoa taarifa mara moja kwa viongozi husika pindi watakapogundua watu wanaojihusisha na suala la ukahaba na ndoa za jinsia moja huku akisema mkoa wa Njombe bado hajaweza kubaini matendo hayo na kuwaagiza viongozi wa serikali kuchukua hatua juu ya suala hilo.
Kwa upande wao Wachungaji na mapadre Wilayani Njombe wamekemea vikali suala la ndoa za jinsia moja,ukahaba na mavazi wanayovaa wafanyakazi wa biashara za pombe za vileo hususani wauzaji baa na vijana wa kiume kuvaa suluari chini ya makalio jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kuhatarisha maisha ya watoto na kuwadharirisha wakristo wilayani hapa na nchini kote.
Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wachungaji na mapadre makanisani mwao mchungaji Evarist Mayala na Cefania Tweve kutoka makanisa ya TAG Tanzania wamesema kuwa suala la ndoa za jinsia moja mbele za Mungu ni Machukizo na kuwataka wanasiasa,wakristo na wananchi kutokubaliana na kitendo hicho cha kusaini mkataba wa kuruhusu ndoa hizo.
Wakizungumza kwa upande wao wananchi mjini Njombe wameomba serikali kutokubaliana na suala la kusaini mkataba wa ndoa za jinsia moja kwa kutegemea misaada toka mataifa ya nje huku wakitaka kuchukuliwa kwa hatua kali dhidi ya makahaba na wanaoendekeza kuvaa mavazi yanachora maumbile yao na chini ya kiuno.
No comments:
Post a Comment