Saturday, April 19, 2014
WANNE WASHIKILIWA NA POLISI KWA WIZI WA NYAYA ZA UMEME
HAWA NDIYO VIJANA WALIOHUSIKA NA WIZI WA NYAYA ZA UMEME MJINI NJOMBE
NA GABRIEL KILAMLYA
Shirika la Umeme Tanesco Wilaya ya Njombe Leo Limefanikiwa Kuwanasa Watu Wawili
Waliokutwa Wakiiba Nyaya za Umeme Katika Kituo cha Kusambazia Umeme Yaani Power
Station Mjini Njombe Huku Wawili Wakihusika Katika Tuhuma Tofauti Ikiwemo Ya
Kununua Nyaya Hizo na Mmoja Kushindwa Kuwajibika Kama Mlinzi wa Zamu.
Tukio Hilo Limetokea Majira ya Saa Nne Asubuhi Huko Katika Mtaa wa Uzunguni Kwenye
Kituo Hicho cha Umeme Yaani Power Station Ambapo Vijana Wawili Wamekatwa na
Mmoja Ametokomea Kusiko Julikana Wakati Wa Msako Huo.
Akizungumza Mara Baada ya Kuwafikisha Kwenye Kituo cha Polisi Mjini Njombe
Msimamizi wa Shirika la Umeme Wilaya ya Njombe Bwana Renatus Henerico Amesema
Kuwa Wizi wa Nyaya Hizo Ulianza Tangu Wiki Iliyopita Lakini Kutokana na Kuweka
Mtego wa Kuwanasa Wezi Hao Leo Zoezi Hilo Limefanikiwa.
Bwana Renatus Amewataja Watuhumiwa Hao Kuwa ni Pamoja na Justin Kyando Mwenye
Umri wa Miaka 17 Mkazi Wa Ramadhani Mjini Njombe,Gehazi Kilumbe Mwenye Umri wa
Miaka 18 Ambaye naye ni Mkazi wa Mtaa Huo wa Ramadhani,Felista Ngota Ambaye ni
Mnunuzi wa Nyaya Hizo Pamoja na Anna Mhenga Ambaye Alikuwa Mlinzi wa Zamu
Katika Lindo Hilo.
Aidha Amemtaja Castory Mligo Kuwa Ametoroka wakati Wa Tukio Hilo na Kwamba
Miongoni Mwa Vijana Hao Wawili Walikuwa Wafanyakazi wa Mkataba Mfupi Katika
Shirika Hilo Yaani S.T.E Ambapo Baada ya Mkataba Wao Kuisha Wakaanza Kujihusisha
na Matukio Hayo.
Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Nyaya Hizo Zilizo Ibiwa Hadi Sasa
Zinagharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni 60 Kwani Walianza Kuiba Tangu Siku Nyingi.
Upands Radio Imefanikiwa Kuzungumza na Mmoja wa Watuhumiwa Hao Anayefahamika
Kwa Jina la Justin Kyando Ambaye Amesema Kuwa Wamekuwa Wakiiba Nyaya Hizo na
Kuziuza Kwa Mfanyabiashara Huyo Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Vyuma Chakavu
Katika Mtaa wa Msichoke Mkabala na Chuo Kikuu cha Amani Mjini Njombe.
Bwana Christian Mlelwa ni Mkuu wa Ulinzi Katika Kampuni Ya Jirani Security Group
Yenye Makao Makuu Yake Jijini Dar es Salaam Ambaye Amesema Amekuwa Akimuomba
Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Kumuongezea Walinzi Hususani Katika Eneo Hilo la Power
Station Lakini Hakuna Utekelezaji Wowote Kwani Eneo Hilo ni Kubwa Zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment