MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI MJINI MAKAMBAKO KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA CHANJO
Wazazi Mkoani Njombe Wametakiwa Kuhakikisha Chanjo ya Matone Kwa Watoto
Waliochini Ya Umri wa Mwaka Mmoja Inatolewa Kwa Watoto Hao Kwa Ajili ya Kinga ya
Magonjwa Nyemelezi Pamoja na Magonjwa Ambukizi Ili Kuepusha Vifo Vinavyotokana
Magonjwa Hayo.
Rai Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi,Sarah Dumba Katika Uzinduzi wa
Wiki ya Chanjo Kitaifa Ambapo Kwa Mkoa wa Njombe Yanafanyika Katika Halmashauri ya
Mji Wa Makambako Ambapo Amesema Kuwa Kila Mzazi Anatakiwa Kuhakikisha Mtoto
Anapata Chanjo ya Matone Ili Kutekeleza Sera ya Taifa Pamoja na Kuwakinga Watoto Na
Magonjwa Shambulizi Kwa Watoto Wenye Umri wa Mwaka Mmoja.
Bi,Dumba Amesema Kuwa Sababu za Kufanya Wiki ya Chanjo Kitaifa Ni Kuhamasisha
Watu Woye Nchini Ili Wahakikishe Watoto Wanaostahili Kupata Chanjo Hiyo Wanapatiwa
Ili Kuwakinga Na Magonjwa yanayozuilika Kwa Chanjo,Kama Hapa Anavyosema,
Aidha Katika Risala Iliyosomwa na Afisa Afya Mkoa wa Njombe Bi,Linda Chatila Kwa
Mgeni Rasmi Bi,Dumba Imeleza Changamoto Mbalimbali Inayokabiliwa Nayo Idara ya
Afya Katika Mkoa wa Njombe, Kama Hapa Anavyosoma.
Pamoja na Mambo Mengine Risala Hiyo Imeeleza Mikakati Ambayo Inatarajia Kufanyika
Katika Idara ya Afya Kuwa ni Pamoja na Kuhakikisha Kila Kituo Kinatoa Huduma ya
Chanjo,Kuwajengea Watoa Huduma Hiyo Uwezo Wa Kutoa Huduma Bora Kwa
Jamii,Kujenga Maabara Bora ya Mkoa Pamoja na Kutoa Elimu Kwa Jamii Namna ya
Kukabiliana Na Magonjwa Yanayoweza Kuzuilika Kwa Chanjo.
Kwa Upande WakeMratibu wa Uzazi na Mtoto Mkoa wa Njombe Bi,Felisia Hyera Amesea
Kila Mzazi Anatakiwa Kuhakikisha Mtoto Anakamilisha Kupata Chanjo Zote Tano Kabla
Ya Kufikisha Umri wa Mwaka Mmoja Ili Kumkinga Dhidi ya Magonjwa Hayo Yanayoweza
Kuzuilika.
Kauli Mbiu ya Wiki ya Chanjo Kitaifa Inasema"CHANJO NI JUKUMU LETU SOTE"
Ikienda Sambamba Pamoja na Ujumbe Unaosema"JAMII ILIYOKAMILISHA CHANJO
NI JAMII YENYE AFYA BORA"
No comments:
Post a Comment