Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limesema Litawachukulia Hatua za Kisheria Wale Wote Watakaobainika Kujichukulia Sheria Mkononi Huku Likiwataka Wananchi Kuwafikisha Kwenye Vyombo Vya Sheria Wahalifu Pindi Wanapowakamata.
Kauli Hiyo ya Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Inakuja Kufuatia Matukio ya Wananchi Kujichukulia Sheria Mkononi Yakiwemo ya Wananchi Kuwaadhibu Wahalifu , Kujinyonga na Kunywa Sumu.
Akizungumza Kwaniaba ya Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe, Mnadhimu wa Jeshi Hilo Focus Mlaengo Amesema Kuwa Vitendo Hivyo Havipaswi Kufumbiwa Macho na Wale Wote Watakaobainika Kujichukulia Sheria Mkononi Kwa Makusudi Hatua za Kisheria Zitachukuliwa Dhidi Yao, Kama Anavyoeleza.
Katika Hatua Nyingine Jeshi Hilo Limesema Linaendelea na Kufanya Uchunguzi wa Tukio la Gari Kubwa Aina ya Benzi Lenye Namba za Usajili T.508 CFD Likiwa na Tella Lenye Namba za Usajili T.428 CBJ Lililowaka Moto na Kuteketea Kibini ya Nyuma Iliyokuwa Imepakia Makaa ya Mawe Ikitokea Songea.
Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Machi Tano Mwaka Huu Majira ya Saa Tatu Usiku Katika Eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi Mjini Njombe Barabara ya Njombe Songea.
Amesema Gari Hilo Ambalo ni Mali ya Crane Transport Ta Dar Es Salaam Lililokuwa Likiendeshwa na Emanuel Mchaka Mwenye Umri wa Miaka 35 Likitokea Songea Likiwa Limebeba Makaa ya Mawe Likielekea Kisumu Nchini Kenya, na Kwamba Katika Tukio Hilo Hakuna Mtu Aliyejeruhiwa , naKueleza Kuwa Chanzo Cha Moto Huo Bado Kinaendelea Kuchunguzwa.
....................................................
No comments:
Post a Comment