HILI NI JENGO LA KIWANDA CHA MAZIWA CEFA NJOMBE AMBALO LINA MITAMBO YA KUTENGENEZA MAZIWA
HIZI NI OFISI ZA UTAWALA WA KIWANDA CHA MAZIWA CEFA NJOMBE
WA UPANDE WA KULIA NI MENEJA WA KIWANDA CHA MAZIWA CEFA NJOMBE EDWIN KIDEHELE AKIMUONGOZA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI. SARAH DUMBA WA UPANDE WA KUSHOTO NA WA KATIKATI NI KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA NJOMBE
VIONGOZI MBALIMBALI WA BODI YA MAZIWA WAKIWA KWENYE KIKAO CHA MAKABIDHIANO YA KIWANDA HICHO LEO
BWANA KAMONGA MKURUGENZI WA CEFA AKIONGEA NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE
MWANASHERIA ADVOCATE SHIMBO AKISOMA SHERIA NA MIONGOZO MBALIMBALI
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIONGEA NA WADAU NA BODI YA MAZIWA LEO WAKATI WA MAKABIDHIANO YA KIWANDA HICHO NA WATU WA CEFA TOKA NCHINI ITALIA
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sara Dumba Hii Leo Amezindua Rasmi Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa Cha Njombe Baada ya Kiwanda Hicho Kukabidhiwa Kwa Wananchi wa Wilaya ya Njombe Kutoka Kwa Wamiliki wa Zamani Kutoka Italia CEFA.
Katika Uzinduzi Huo Pia Bi. Dumba Amewasimika wa Kurugenzi Watano wa Bodi Hiyo Ambapo ni Wawakilishi wa Hisa za Kiwanda Hicho na Kuitaka Bodi Hiyo Kuhakikisha Wanaongeza Kasi ya Uzalishaji.
Akizungumza Katika Uzinduzi Huu Mkuu Huyo wa Wilaya Amewataka Wakurugenzi wa Bodi Hiyo Kuhakikisha Wanakisajili Kisheria Kiwanda Hicho na Kinafanya Kazi Kwa Kushirikiana na Wafugaji Kutoka Katika Umoja Wao wa NJOLIFA Pamoja na Kuacha Kutegemea Wafadhili Kama Ilivyokuwa Mwanzo, na Hapa Anaeleza.
Akitoa Muongozo wa Usimamizi wa Kiwanda Hicho Ambacho Kwa Sasa Kinafanya Kazi Kibiashara na Si Kama Mradi, Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Dustan Shimbo Amesema Kuwa Kiwanda Hicho Kinatakiwa Kufuata Sheria za Kibiashara Ikiwemo Kulipa Kodi Serikalini,Kutoa Ajira Kwa Wazawa Pamoja na Kushiriki Kwa Kutoa Misaada Kwa Jamii Kama Wawekezaji Wengine.
Kwa Upande Wake Meneja wa Kiwanda Hicho Edwin Kidehele Amesema Kuwa Bao Wanakazi ya Kuhakikisha Wanaboresha Bidhaa Zinazozalishwa Katika Kiwanda Hicho Pamoja na Kutatu Changamoto Zinazokikabili Kiwanda Hicho Ikiwemo Baadhi ya Wafugaji Kufuga Pasipo Kufuata Kanuni za Ufugaji Bora .
No comments:
Post a Comment