Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, March 11, 2014

MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WANOLEWA NJOMBE






 MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WAKIKABIDHI ZAWADI KWA MGENI RASMI





 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI. SARAH DUMBA AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKIWA MGENI RASMI KATIKA KUHITIMISHA MAFUNZO HAYO LEO
 MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKITOA HOTUBA YAKE KWA WAMILIKI NA MADEREVA  MAFUNZO YALIOHITIMISHWA LEO KATIKA UKUMBI WA TURBO MJINI NJOMBE

 WA UPANDE WA KULIA MKUU WA MKOA WA NJOMBE WA KATIKATI NI MKURUGENZI WA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA APEC NA KUSHOTO KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE











 MSANGI AKITOA ONYO KWA WAMILIKI NA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI KWA KUPUNGUZA AJALI.

 KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI AKISHUKURU SHIRIKA LA APEC KWA KUTOA MAFUNZO HAYO NJOMBE PAMOJA NA MADEREVA KUHUDHURIA KWA WINGI KUSHIRIKI MAFUNZO HAYO




MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI SARAH DUMBA AKIWA UKUMBI WA TURBO WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YA UDEREVA KWA MADEREVA MKOANI NJOMBE

Mkuu wa mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Aseri Msangi amewataka wamiliki na madereva wa vyombo vya moto kujiunga katika vikundi ili kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa kuku wa mayai na nyama kwaajili ya kuinua uchumi wa kila mmoja.

Akizungumza na wamiliki na madereva wa vyombo vya moto wakati wa kufunga mafunzo ya udereva yaliotolewa kwa muda wa siku saba Mkuu wa mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Aseri Msangi amewataka wamiliki na madereva hao kuwa wabunifu na kutafuta njia mbalimbali za kuendeleza miradi yao ikiwemo kujiunga kwenye Banki za Wananchi Vijijini VIKOBA  Na SACCOS ili kuongeza kipato na uchumi wao.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo Captain Msangi amesema kuwa madereva pamoja na wananchi mkoani Njombe wanayo fursa kubwa ya kupatiwa mikopo nafuu kupitia vikundi watakavyo uunda  jambo ambalo litasaidia kuinua uchumi wao kwa kuendeleza miradi ya kilimo na rasilimali zilizopo miongoni mwao kwa kujiimarisha kifedha ambapo endapo watazingatia masharti ya mikopo na urejeshaji kuzingatiwa watanufaika na mikopo hiyo.

Msangi amesema kuwa wamiliki na madereva wa Vyombo vya moto wanatakiwa kujenga mahusiano mazuri na vyombo vya utumishi Ikiwemo polisi,TRA,Halmashauri na Sumatra  ili kwenda sambamba na matakwa ya serikali katika kufanikisha mipango na mikakati ambayo imekuwa ikiwekwa kwaajili ya kukuza mapato ya serikali.

Amesema  kuwa kwa mujibu wa sheria ya Sumatra ya Mwaka  2009  inaruhusu vyombo vya usafiri aina ya bajaji kubeba abiria kwa kukodishwa tu na siyo vinginevyo ambapo sheria hiyo ya mwaka 2009 iliruhusu bajaji na pikipiki kufanya kazi kama vyombo vingine kwa kukodishwa katika vituo maalumu  ili kuepuka mwingiliano na kusababisha ajali za barabarani.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa huyo amewataka madereva hao kujiunga katika mfuko wa bima ya Afya CHF na mifuko mingine ya Bima ya afya ili waweze kupatiwa matibabu bure pindi wapatapo tatizo la ugonjwa.

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amesema kuwa usafiri wa bajaji hauruhusiwi kubeba mtoto mwenye umri wa chini ya miaka tisa akiwa peke yake pasipo mtu mzima huku akisema usafiri wa pikipiki hautakiwa kubeba zaidi ya abiria mmoja wakati wa kufanya kazi zake.

Kamanda Ngonyani amesema kuwa wamiliki na madereva  wa pikipiki wanatakiwa kuzingatia masharti ya uendeshaji wa vyombo hivyo kwa kuvaa vifaa vya pikipiki ikiwemo kofia ngumu {heremetes} na nguo mbalimbali za kusitili mwili wake kama dereva.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la APEC Bwana Restipishasti  Manya amesema kuwa jumla ya wahitimu wa mafunzo ya udereva  131 wamepatiwa vyeti ya kuhitimu mafunzo hayo ambapo wanatakiwa kufuatilia Leseni zao katika Halmashauri ya mji wa Njombe ili kufanya kazi zao za barabarani pasipo kusumbuliwa na maafisa usalama wa barabarani.

Bwana Manya amesema kuwa lengo la shirika hilo kutoa mafunzo kwa madereva wa vyombo vya moto hususani pikipiki ni kutaka kuweka mahusiano kati ya viongozi wa serikali na madereva hao ambapo pamoja na mambo mengine amesema pia kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikitokea na kuibiwa kwa vyombo hivyo hapa nchini.

Amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa kushirikiana na Uongozi wa jeshi la polisi,halmashauri  ambapo mafunzo hayo nyameonesha tija kwa madereva huku akisema kuwa taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo projetors,mwitikio mdogo wa walengwa na miundo mbinu ya barabara.

Akisoma risala fupi katibu wa wamiliki na madereva wa pikipiki mjini Njombe bwana Emiramu Msigwa amesema kuwa mafunzo hayo yamewapoatia manufaa makubwa madereva hao huku akisema kuwa madereva hao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kukabwa na kuibiwa pikipiki zao,ugumu wa kupatikana kwa leseni,waendesha baiskeli na mikokoteni kutokuwa na elimu ya usalama wa barabarani pamoja na madereva wa magari makubwa kuto wathamini wakiwa barabarani ambapo wamekuwa wakiwachomekea ghafra na kusababisha ajali.

Hata hivyo madereva hao wameomba serikali kuwatekelezea mahitaji mbalimbali ikiwemo kupatikana kwa leseni kwa urahisi,madereva wa magari wanaowachomekea wachukuliwe hatua,shirika la APEC wameomba lirudi tena kutoa mafunzo kwa wale ambao hawajabahatika kupatiwa mafunzo hayo,pia bodaboda wamejipanga kuto shiriki vurugu pamoja na halmashauri ya mji kuombwa kuongeza alama za barabarani kwa baadhi ya maeneo ambayo hayana alama hizo.




No comments:

Post a Comment