Kauli
hiyo ya pamoja imetolewa jana wilayani Nkasi na wanaharakati wa mtandao
huo walipokuwa katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya Utepe Mweupe wilayani
hapa, mkoani Rukwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
‘Evidence for Action’ ambao wanatekeleza mradi ujulikanao kama ‘Mama
Ye’, Craig John, alisema wamepata malalamiko toka kwa wananchi ya kuwa
kuna tabia ya baadhi ya watendaji kwenye sehemu za kutolea huduma za
afya huwauzia wagonjwa damu kitu ambacho hakikubaliki.
“...Wakati
tunapita pita mitaani kuhamasisha wananchi kuja kujitolea damu kwa
ajili ya akinamama wajawazito wanaohitaji kuongezewa damu, wananchi
walituambia kuwa baadhi ya watendaji wa afya wamekuwa kero kwao kwani
wanawauzia damu pindi wanapokuwa wanaihitaji,” alisema Craig.
Naye Mratibu wa Utepe Mweupe nchini, Bi. Rose Mlay aliitaka serikali
kutenga bajeti mahususi katika mwaka wa fedha 2014/2015 ili kuhakikisha
vituo vya afya wanatoa huduma za dharura ikiwemo upasuaji na damu
salama.
“...kama
mtoto amekaa vibaya tumboni kwa mama au hata kama amepigwa mwanamke
huyu anaweza kusaidiwa kwa kufanyiwa upasuaji na kuongezewa damu salama
pekee, hivi ndivyo vitakavyo muokoa,” alisema Rose.
Sherehe za kilele cha Wiki ya Utepe Mweupe zinatarajiwa kufanyika Machi
15, 2014 wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.
No comments:
Post a Comment