Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, March 9, 2014

MIRADI MITATU YA ELIMU YAWEKEWA MAWE YA MSINGI KATA YA MTWANGO WILAYANI NJOMBE



 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIONGEA NA WANANCHI MTWANGO SIKU YA KUWEKA MAWE YA MSINGI KWENYE MIRADI YA ELIMU KATA YA MTWANGO

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Ameweka Mawe ya Msingi Katika Miradi Mitatu ya Elimu Katika kata ya Mtwango Ambapo Amewataka Wananchi wa Maeneo Inayotekelezwa Miradi Hiyo Kuhakikisha InaKamilika Kwa Wakati na  Kuboresha Mazingira ya Kijifunzi na Kufundishia.

Miongoni Mwa Shule Zilizowekewa Mawe ya Msingi ni Shule Mpya Mbili za Msingi za Inyamalwa Iliyopo Itunduma na Limakwale Katika Kijiji cha Ilunda Pamoja na Nyumba ya Mwalimu Shule ya Sekondari Sovi, Miradi Yote Ikiwa na Thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 134.

Akizungumza na Wananchi wa Vijiji Vya  Ilunda, Lunguya na Itunduma Kwa Nyakati Tofauti Bi. Dumba Amewapongeza Wananchi na Viongozi Kwa Kushirikiana Katika Miradi ya Maendeleo Ambapo Pia Ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kwa Kuhamasisha na Kushirikiana na Wananchi na Serikali Zao za Vijiji .

Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Amewataka Viongozi wa Serikali za Vijiji , Wananchi Pamoja na  Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Hiyo Kuhakikisha Wanasimamia Kikamilifu Misaada na Fedha Kwa Ajili ya Kusimamia Miradi ya Maendeleo, Kama Anavyoeleza.

Kwa Upande Wake Afisa Elimu Ufundi wa Halmashauri Hiyo Mwalimu Humphery Milinga Amewataka Wazazi na Walezi wa Wanafunzi Katika Vijiji Hivyo Kuendelea Kuchangia Chakula Shuleni, Huku Akiwataka Viongozi Kuwachukulia Hatua za Kisheria Wazazi na Walezi Wanaokaidi Kuchangia Chakula Shuleni , na Hapa Anaeleza.

Ziara Hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Siku Moja Katika Vijiji Vya  Ilunda, Lunguya na Itunduma
Ililenga Kuweka Mawe ya Msingi Katika Miradi Hiyo Pamoja na Kuwahamasisha Wananchi Kushiriki Katika Miradi Inayotekelezwa Katika Maeneo Yao.

No comments:

Post a Comment