Sunday, March 9, 2014
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UNYANYASAJI WA KIJINSIA NJOMBE
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIWA MGENI RASMI KWENYE SHEREHE ZA WANAWAKE KIWILAYA KWA WILAYA YA NJOMBE YALIFANYIKIA KIJIJI CHA WELELA
Serikali Wilayani Njombe Imesema Itaendelea Kupambana na Vitendo Vya Unyanyasaji na Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Wakike Vinayofanywa na Baadhi ya Wananchi Ndani ya Jamii.
Kauli Hiyo ya Imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi, Sara Dumba Wakati Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Welela Kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Huku Akiitaka Jamii Kuachana na Dhana Potofu za Kuwakandamiza Wanawake Pamoja na Kuwarithi Wajane .
Mkuu Huyo wa Wilaya Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi Amesema Kumekuwa na Taarifa
Zinazoeleza Jinsi Wajane Wanavyolazimishwa Kurithiwa Huku Wengine Wakinyanyaswa Kwa Kunnyang'anywa Mali Pamoja na Kufanyiwa Vitendo Vya Ukatili Hali Inayosababisha Wanawake Hao Kuishi Katika Mazingira Magumu.
Katika Taarifa Fupi Iliyosomwa Mbele ya Mkuu wa Wilaya Imesema Kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii Imekuwa Ikitoa Kipaumbele Kwa Wanawake Kwa Lengo la Kuwakwamua Kiuchumi Pamoja na Kushughulikia Baadhi ya Kesi Zikiiwemo za Wanaume Kuzitelekeza Familia Zao.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Welela Wamesema Licha ya Serikali Kuwa na Sera ya Kuwathamini Wanawake Lakini Bado Kuna Baadhi ya Changamoto Zinazowakabili Wanawake Zikiwemo za Kunyanyaswa Huku Baadhi ya Viongozi Wakishindwa Kuzitatua Changamoto Hizo.
Maadhimisho ya Siku wa Wanawake Duniani Huadhimishwa Machi Nane Kila Mwaka Ambapo Kwa Mwaka Huu Yameadhimishwa Kitaifa Jijini Dar Es Salaam na Kwa Wilaya ya Njombe Yameadhimishwa Katika Kijiji cha Welela Kata ya Mtwango na Kuhudhuriwa na Viongozi Mbalimbali Pamoja na Wananchi , Chini ya Kaulimbiu Isemayo”Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment