MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MADILU BI. DEOKALA MLWILO AKIZUNGUMZA NA WANANCHI
WANANCHI WA KIJIJI CHA MADILU WILAYANI LUDEWA WAKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA WA KIJIJI HICHO
MWENYEKITI WA SHIRIKA LA ILAWA IPROVEMENT ORGANIZATION LINALOHUSIKA NA UTUNZAJI WA KAZINGIRA NATHANAEL MGAN AKITOA ELIMU JUU YA UTUNZANI WA MAZINGIRA KIJIJINI HAPO
Serikali ya Kijiji cha Madilu Wilayani Ludewa Imefanikiwa Kukusanya Zaidi ya Shilingi Milioni Kumi Katika
Kipindi cha Miezi Mitatu Kutoka Katika Miradi ya Serikali Hiyo.
Akisoma Taarifa ya Mapato na Matumizi Kwenye Mkutano wa Hadhara Afisa Mtendaji wa Kijiji Hicho Bony
Teodor Nzikalila Amesema Mapato Hayo Yametokana na Mauzo ya Msitu wa Miti na Gari Lililokuwa Mali ya Kijiji
cha Madilu , Ushuru wa Maduka na Vibanda Vya Biashara Pamoja Vilabu Vya Pombe za Kienyeji.
Akielezea Matumizi ya Fedha Hizo , Afisa Mtendaji Huyo Amesema Zaidi ya Shilingi Milioni Saba
Zimetumika Katika Matumizi Mbalimbali Ikiwemo Kununulia Vitabu Vya Ofisi na Matumizi Mengine ya
Kijiji Hicho , Huku Kiasi Kilicho Salia Kimehifadhiwa Katika Akaunti ya Kijiji Hicho .
Katika Hatua Nyingine Bwana Teodor Amewaomba Wananchi Kuendelea Kuchangia Miradi Mbalimbali ya
Maendeleo Inayotekelezwa Katika Kijiji Hicho Ukiwemo Mradi wa Maji Ambao Ukikamilika Utamaliza
Changamoto ya Upatikanaji wa Huduma ya Maji Safi na Salama.
Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Baadhi ya Wananchi Wameitaka Serikali ya Kijiji Hicho Kusitisha
Kwa Muda Kutumia Fedha Zitokanazo na Rasilimali za Kijiji na Zile Zinazochangwa naWananchi Hadi Hapo
Uchaguzi Unaotarajia Kufanyika Utakapokamilika na Kwamba Fedha Ndipo Zianze Kutumika Katika
Utekelezaji Miradi.
Aidha Wananchi Hao Wamesema Wamechukua Hatua Hiyo Kutokana na Kutokuwa na Imani ya Serikali
Hiyo Kwa Kile Walichokidai Kuwa Uongozi Huo Umekuwa na Matumizi Mabaya Hali Inayo Sababisha
Baadhi ya Miradi Kutokamilika Kwa Wakati.
No comments:
Post a Comment