Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, March 5, 2014

DC NJOMBE AWATAKA VIONGOZI WA VIJIJI KUSOMA TAARIFA ZA MAPATO.



 MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKIJIBIA  KUHUSU MTENDAJI WA KATA KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA MADAWATI YA SHULE YA MSINGI LUNGUYA

 MTENDAJI WA KATA YA MTWANGO AKIJIBIA MALALAMIKO YA WANANCHI YA KUMTUHUMU KUHUSIKA NA UBADHILIFU WA FEDHA ZA MBUNGE ALIZOAHIDI KUZITOA

 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI. SARAH DUMBA AKITATUA MGOGORO ULIOPO BAINA YA OFISI YA KIJIJI,KATA  KWA KUSHINDWA KUWASHIRIKISHA WAKATI WANABINAFSISHA SOKO LA MBAO PAMOJA NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA MIRADI YA KIJIJI HICHO.









 RHODA MAHAVA MUHASIBU HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKIJIBU BAADHI YA MASWALI AKIWA NA MWENZAKE RICHARD KOMBA KWA MASWALI YANAYOWAHUSU


 RICHARD KOMBA AKISOMA SHERIA ZA USHURU






Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sarah Dumba amesema kuwa amebaini udhaifu mkubwa wa kiutendaji uliopo katika serikali ya kijiji cha Lunguya kata ya Mtwango Wilayani Njombe na kuwataka viongozi wa kijiji hicho kuhakikisha wanawasomea hesabu za mapato na matumizi wananchi ili kuondoa migogoro baina yao.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lunguya Bi. Dumba amesema kuwa udhaifu mwingine alioubaini ni pamoja na kuitishwa kwa mkutano wa hadhara wa kuadhimia kutengua wajumbe wa serikali ya kijiji na kwamba mkutano huo ulikuwa batili kwa kuwa haukufuata sheria huku akisema kutofanyika kwa mikutano ya kisheria imepelekea kuwepo kwa malumbano yanayosababishwa na udhaifu wa kutendaji wa kiuongozi.

Aidha bi.Dumba amesema kuwa wananchi wa kijiji cha Lunguya wanatakiwa kufuata sheria kwa kuitisha mkutano wa hadhara ili kumhoji hadharani afisa mtendaji wa kata na kijiji hicho ajibu tuhuma za wizi wa fedha mbele yao na ikiwezekana wabadilishe uongozi mzima wa kijiji na kukaimisha viongozi wengine watakao simamia shughuli za maendeleo ya kijiji pamoja na kujenga hoja za msingi katika kutafuta haki yao.
Bi. Dumba amesema kuwa pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kutothubutu kumkaribisha kiongozi ama mtu yeyote mwenye maslahi binafsi katika miradi ya serikali ya kijiji  na kuwataka wananchi kumpeleka kwenye vyombo vya sheria afisa mtendaji wa kata hiyo kwa tuhuma anazodaiwa kutumia vibaya fedha za kijiji shilingi laki sita zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini.


Akitolea ufafanuzi kuhusiana na fedha ambazo wanamtuhumu afisa mtendaji wa kata ya Mtwango bwana Jimson Simwanza mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe Paulo Malala amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutuma taratibu za kisheria kumufikisha polisi endapo wanamtuhumu mtendaji huyo kuhusika na ubadhilifu wa fedha hizo ili hatua kali zichukuliwe dhidi yake kuliko kuishia kulalamika  kwa viongozi wengine huku mtuhumiwa wnamfahamu.

Awali wananchi wa kijiji cha Lunguya walilalamikia kushindwa kuchukuliwa kwa hatua za haraka za kisheria dhidi ya mtendaji wa kata ambae wanamtuhumu kutumia fedha za madawati kwa maslahi yake, Halmashauri kutorudisha asilimia ya mapato ya ushuru wa mbao,hesabu za mapato na matumizi ya kijiji kutosomwa,kuwekwa kwa mdhabuni wa kutoza ushuru wa mbao pasipo wananchi kujulishwa utaratibu uliopo pamoja na ushuru wa kifusi cha kujengea barabara kutopelekwa kwenye serikali  ya kijiji Jambo ambalo halmashauri imekili kuwepo kwa mapungufu hayo.

No comments:

Post a Comment