Monday, March 3, 2014
WANAWAKE WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA FAMILIA ZAO
MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG MELINZE NJOMBE AKIINGIA NA MAMA MCHUNGAJI KANISANI HAPO BAADA YA MKUU WA WILAYA KUWASILI
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKITOA HOTUBA YAKE KATIKA KANISA LA TAG MELINZE NJOMBE KWENYE SKUKUU YA WANAWAKE WATUMISHI WA KIKRISTO WA TAG MELINZE.
HUYU NI MZEE WA KANISA KIONGOZI TAG MELINZE BWANA DANIS DAMAS MWAKABULI AKIZUNGUMZIA SUALA LA MAADILI KWA VIJANA KATIKA KANISA
KWAYA YA AKINA MAMA WAKITUMBUIZA KANISANI HAPO KWA FRAHA,SHANGWE NA NDEREMO BAADA YA MKUU HUYO WA WILAYA KUITIKA WITO WAO.
AKINA MAMA WA KANISA LA TAG BAADA YA KUKABIDHI ZAWADI KWA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE HAWA NI WAWAKILISHI TU WAPO KWENYE PICHA YA PAMOJA
VIONGOIZI WA KANISA TAG MELINZE NJOMBE WAKIWA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI AKIWEMO MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA NA KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA WA NJOMBE ERNEST MKONGO.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe bi. Sarah Dumba amewataka wanawake kutekeleza wajibu wao katika malezi ya jamii kwa kuwataka kujikita katika miradi ya kiujasilia mali ili kujikwamua kiuchumi pamoja na kuzitunza familia zao katika misingi ya maadili ya kidini.
Ameyasema hayo Akiwa mgeni rasmi kwenye Sikuu ya waumini wa kanisa la Tanzania Assemblis Of God TAG mjini Njombe na kusema kuwa baadhi ya wakristo wamekuwa hawazingatii mafundisho ya kidini ambayo yamekuwa yakitolewa makanisa huku akisema wanawake wananafasi kubwa ya kukemea tabia mbalimbali ikiwemo Imani za kishirikiana zinazosababisha vifo vya watu wengi,dhuluma,fitina na mauaji.
Aidha bi Dumba amesema kuwa baadhi ya wanawake na familia zao wamekuwa wakinyanyasika na wanaume kwa kuwatelekeza na kusababisha kuishi katika mazingira magumu kwa familia ambapo amewataka wakristo kutotumia nafasi ya mahubiri ya kidini kuficha uovu wao kwani wanawake ndiyo nguzo kuu ya kuhakikisha uovu huo hautokei katika jamii.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa wanawake wamrudie Mungu katika kutii mamlaka zilizopo na kutimiza majukumu yao ya malezi na ustawi wa Jamii kwa kuwa na umoja kupitia kumuamini Mungu kupata ukombozi wao kwa kuwalea vizuri watoto wao.
Akisoma risala fupi mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Njombe Katibu wa wanawake watumishi wa wa Kikristo wa kanisa la TAG Bi.Marina Mbugi amesema kuwa lengo la kuanzisha chama cha umoja wanawake wa kikristo lilikuwa ni kuhamasisha wanawake kujihusisha katika miradi mbalimbali ya kilimo,ufugaji na shughuli za kijasilia mali pamoja na kufanya maombi ya kupeleka baraka njema katika familia zao.
Awali akimkaribisha mkuu wa Wilaya ya Njombe Mchungaji wa kanisa la TAG Mchungaji Cefania Tweve amempongeza mkuu huyo kwa kuitika wito na kusema kuwa ni kiongozi bora kwani anasikiliza matatizo ya kila mtu pasipo ubaguzi.
Mkuu wa Wilaya huyo jana amekagua miradi ya ujasiliamali ya wanawake watumishi wa kikristo wa kanisa la TAG Melinze ikiwa ni moja ya kuhamasisha kujikita katika shughuli za maendeleo katika wiki hii ya kuelekea kilele cha sherehe za Wanawake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment