NA HAWA NI KUKU WA KISASA WA MJASILIAMALI HUYO
HAWA NI KUKU WA KYENYEJI
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI TITUS KAMANI AKIWA KATIKA MABANDA YA MFUGAJI KIJIJI CHA WIKICHI MJINI NJOMBE
HUYU NI MFUGAJI WA KUKU,NG'OMBE NA SAMAKI M JINI NJOMBE BWANA MGIMBA
WAZIRI KAMANI AKIKAGUA MABWAWA YA SAMAKI MJINI NJOMBE
HAYA NI MABWAWA YA MFUGAJI HUYO WA KIJIJI CHA WIKICHI MJINI NJOMBE BWANA MGIMBA
WAZIRI KAMANI
Waziri wa maendeleo ya mifugo na Uvuvi Dkt Titus Kamani ameupongeza uongozi wa mkoa wa Njombe na halmashauri zake kwa jitihada mbalimbali wanazozifanya za kutekeleza miradi kwa manufaa ya jamii na kizazi cha baadae kwa kuhimiza chakula na unywaji wa maziwa shuleni pamoja na ufugaji wa mifugo ya ng'ombe wa maziwa na wasiyo wa maziwa,kuku,samaki na mifugo mingine.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikelu mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa kwenye ziara ya siku tatu mkoani Njombe Waziri Kamani amesema kuwa amefurahishwa kuona shule mbalimbali mkoani hapa zimeingizwa kwenye mpango wa kutumia maziwa jambo ambalo litasaidia kuongeza ufahamu katika masomo na ufauru kwa wanafunzi.
Aidha Dkt Kamani amesema kuwa mpango huo wa unywaji wa maziwa umewekwa kitaifa licha ya kuwa haupo mikoa yote ambapo amewashukuru wazazi kwa kukubali kuchangia mchango wa unywaji wa maziwa shuleni na kuwataka kuendelea na mpango huo kwani maziwa yanaongeza uwezo wa kufikiri huku akiziomba serikali za vijiji kuhamasisha mpango huo wa kupewa maziwa nyumbani na shuleni.
Hata hivyo waziri Kamani akiwa katika mradi wa ufugaji wa kuku na Samaki wa mjasiliamali wa kijiji cha Wikichi mjini Njombe amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutembelea miradi inayotekelezwa na baadhi ya wajasiliamali ili kujifunza na kuiga mfano huo na kwamba wanatakiwa kujikiti katika ufugaji wa kuku na kuanzisha mashamba darasa kwaajili ya kujikwamua kiuchumi Ambapo changamoto ya kukosekana kwa wataalamu wa Samaki akaahidi kwenda kulitafutia ufumbuzi.
Katika taarifa yake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikelu bwana Danny Mhema amesema kuwa kumekuwa na imani potofu juu ya unywaji wa maziwa ambapo baadhi ya wazazi wamekuwa wakiamini kuwa mradi wa maziwa ni wakujinufaisha kwa walimu na wazalishaji wa maziwa jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa uchangiaji mdogo kwa baadhi ya wazazi .
Katika Risala ya mfugaji wa kuku,samaki na Ng'ombe bwana Aidan Mngimba amesema kuwa ana jumla ya kuku wa asili mia sita na kuku wa mayai elfu moja mia sita ikiwa alianza na kuku watano mwaka 2004 na mwaka 2005 alianza kufuga ng'ombe watano wa kyenyeji ambapo kutokana na kukosekana kwa maeneo ya kuchungia aliamua kufuta mradi huo na kuanzisha mradi wa ng'ombe wa kisasa kwaajili ya maziwa.
No comments:
Post a Comment