Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, March 22, 2014

UVIKIDA WAKABIDHI DARASA KIBENA


KATIBU WA UMOJA WA VIJANA KIBENA WANAOISHI JIJINI DAR ES SALAAM BWANA  ZAWAD NYEKELELA CHOTA AKIKATA UTEPE

WA UPANDE WA KULIA NI MGENI RASMI AMBAE NI MRATIBU ELIMU KATA YA NJOMBE MJINI BWANA EGID FRANCIS  MHEMA

MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIBENA MESHAK MNYAWASA




AFISA MTENDAJI WA MITAA MITATU KIBENA HOSPITALI,KIBENA KATI NA MPETO BWANA OTMAR MBANGALA AKISHUKURU KWA NIABA YA WANANCHI WA MITAA HIYO
MGENI RASMI MRATIBU ELIMU NKATA YA NNJOMBE MJINI ALIYEKWENDA KWA NIABA YA AFISA ELIMU HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE MWALIMU EGID FRANCIS MHEMA

KATIBU WA UVIKIDA BWANA ZAWADI NYEKELELA CHOTA AKITOA TAARIFA FUPI MBELE YA MGENI RASMI WAKIWA SHULENI HAPO
KATIBU UVIKIDA AKIKABIDHI UFUNGUA WA MLANGO WA DARASA HILO KWA MGENI RASMI

MGENI RASMI AKIKABIDHI PIA UFUNGUO HUO KWA MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIBENA
MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIBENA MESHAKI MNYAWASA AKISOMA TAARIFA FUPI MBELE YA MGENI RASMI
MGENI RASMI AKITOA HOTUBA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA ZOTE YA MWALIMU NA KATIBU WA UVIKIDA



Umoja wa Vijana Kibena Wanaoishi Mkoani Dar Es Salaam UVIKIDA Leo Wamekabidhi Darasa Moja Walililolifanyia Ukarabati Katika Shule ya Msingi Kibena Ikiwa ni Jitihada Zao za Kuinua na Kuboresha Mazingira ya Elimu Katika Shule Hiyo.

Akiongea Wakati wa Kukabidhi Darasa Hilo Kwaniaba ya Umoja wa Vijana Hao Katibu wa UVIKIDA Zawadi Nyekelela Chota Amesema Wamefanya Hivyo Kwa Lengo la Kurudisha Fadhira Kwa Shule na Eneo Walilozaliwa, na Kusema Kuwa Ukarabati Huo Umeghari Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili.


Akizungumza Mara Baada ya Kupokea Darasa Hilo Kwaniaba ya Afisa Elimu Shule za Msingi Halmashauri ya Mji wa Njombe Egid Francis Mhema Ambaye ni Mratibu Elimu Kata Njombe Mjini Amepongeza Hatua ya UVIKIDA Huku Akiwataka Wananchi na Wadau Wengine Kuiga Mfano wa Vijana Hao.

Aidha Mwalimu Francis Amewataka Wananchi Kushirikiana na Walimu Katika  Kujadili na Kutatua ChangamoTO Mbalimbali Zinazozikabili Shule Nyingi Ili Kuboresha na Kuinua Kiwango cha Elimu Ikiwemo Mikutano Inayoitishwa na Kamati za Shule.

Akiongea Kwaniaba ya Uongozi wa Shule ya Msingi Kibena Mwalimu Mkuu wa Shule Hiyo Meshack Mnyawasa Ameushukuru Umoja Huo Kwa Kuwaisaidia Shule ya Msingi Kibena Kufanya Ukarabati wa Darasa , Ambapo Amewaomba Wahisani Mbalimbali Kuendelea Kuisaidia Shule Hiyo Kutatua Changamoto Zinazoikabili.

Afisa mtendaji wa mitaa ya Kibena hospitali,kibena kati na Mpeto bwana Otmary Mbangala nae akashukuru kwa msaada huo kwa niaba ya wananchi wa mitaa hiyo Kwamba watakwenda kuhamasisha wananchi nao waweze kutambua umuhimu wa kusaidia uboreshaji wa elimu kwa baadhi ya wadau wa elimu.

No comments:

Post a Comment