KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
MTOTO MWENYE
UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HENRY JUMA MKAZI WA MIGOMBANI ALIKUTWA
AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KULAZWA KITANDANI NA BABA YAKE MZAZI
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA VENANCE.
TUKIO HILO LA
KUSIKITISHA LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014
MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO
KATIKA KATA YA MIGOMBANI, TARAFA YA TUNDUMA,
WILAYA YA MOMBA AMBAPO BAADA YA UHALIFU HUO, MTUHUMIWA ALIFUNGA MLANGO KWA NJE
NA KUFULI NA KUTOKOMEA MAHALI KUSIKOJULIKANA. WAPELELEZI PAMOJA NA RAIA
WALIPOVUNJA MLANGO NA KUINGIA NDANI WALIKUTA MAITI YA MTOTO HUYO IKIWA
KITANDANI. KATIKA CHUMBA HICHO WALIKUTA UJUMBE WA MANENO MENGI YALIYOANDIKWA NA
MTUHUMIWA, BAADHI YA MANENO HAYO NI “UNYAMA UNYAMANI, TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE
J.M A.K.A GAIDI”. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
|
No comments:
Post a Comment