Kituo cha Afya Tunduma
Kampuni ya
Bia Tanzania imetoa msada wa kisima cha maji kwa ajili kituo cha Afya Tunduma
chenye thamani ya shilingi milioni 24 chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa.
Afisa
uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya
Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha
fadhila kwa Watanzania.
Malulu
amesema kampuni yake imetenga jumla ya shilingi milioni 450 kwa ajili ya miradi
mbalimbali ya maendeleo nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha yenye nia ya
kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Naye Afisa
mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa amesema mradi huo utasaidia kumaliza tatizo la maji hivyo kuwa faraja kwa
wagonjwa wanaotumia kituo hicho ikiwa ni pamoja na raia wa nchi jirani ya
Zambia.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya
Momba Abiud Saideya amesema kuwa
watahakikisha wanautunza mradi huo ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na
kijacho .
Aidha Diwani
wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka ameshukuru Kampuni hiyo kwa kutoa mradi huo
na hivyo kuwataka wahudumu kuitunza miundo mbinu ya maji.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo ameitaka
kampuni ya bia kupanua wigo wa kusaidia Nyanja nyingine kama vile elimu ili
kufanya mji wa Tunduma kuwa na maendeleo zaidi.
|
No comments:
Post a Comment