Friday, March 14, 2014
TAKRIBANI WAGONJWA 2000 WANAOTUMIA ARV'S HAWAJULIKANA WALIKO NJOMBE
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini TACAIDS Dokta Fatma Mrisho Akihojiwa na Waandishi wa Habari Mkoani Njombe Mara baada ya kuhitimisha Ziara ya Siku Mbili
Dokta Rafael Kalinga Akihojiwa na Wanahabari Katika Msafara wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
Askofu Mstaafu Peter Mwamasika Naye Akizungumza na Vyombo Vya Habari
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini TACAIDS Dokta Fatma Mrisho Ameagiza Kuwafatilia Wagonjwa 2778 Waliokuwa Wakitumia Dawa za Kupunguza Makali ya Virusi Vya Ukimwi Ambao Kwasasa Hawafahamiki Walipo, na Ifikapo Mwezi Nne Mwaka Huu Taarifa Kuhusu Wagonjwa Hao Ziwezimetolewa.
Dokta Fatma Mrisho Ametoa Agizo Hilo Kufatia Taarifa Iliyosomwa na Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Njombe Dkt. Eusibil Kessy Mbele ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini Wakati Tume Hiyo Ilipotembelea Hospitali ya Halmashauri Mji wa Njombe (Kibena) Kuangalia Maendeleo ya Wagonjwa wa
Ukimwi Katika Hospitali Hiyo .
Katika Taarifa Hiyo Imeeleza Kuwa Hadi Sasa ni Wagonjwa 3489 Kati ya Wagonjwa 4946 Ndiyo Wanaotumia Dawa na Kwamba Tayari Mratibu wa Ukiomwi Mkoa wa Njombe Dkt. Eusibil Kessy Ameyaagiza Mashirika Yanayojishughulisha na Masuala ya Ukimwi Yakiwemo ya SHISO na COCODA Kuwafatilia Wagonjwa Hao .
Kwa Upande Wake Mratibu wa Ukimwi Halmashauri ya Mji wa Njombe Dkt. Adelitus Mgao Ameiiomba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Kuwapatia Gari Litakalokuwa Linatumika Kwa Masuala ya Ukimwi Kwani Gari Lililopo Ambalo Lilitolewa na Tunajali na Kwasasa Linatumika na DMO.
Ziara Ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Taifa TACAIDS Imehitimisha Ziara Yake ya Siku Mbili Hapo Jana Ambapo Pamoja na Mambo Mengine Amebaini Changamoto Mbalimbali Zinazosababisha Ongezeko la Maambukizi Mapya ya Virusi Vya Ukimwi Mkoani Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment