MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIBENA NYAWASA AKISALIMIANA NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KIBENA
MAJENGO YA SHULE YA MSINGI KIBENA JINSI YALIVYOCHAKAA NI MADARASA HAYA
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuhakikisha Inafanya Tathmini ya Uchakavu wa Majengo Katika Shule ya Msingi Kebena Ili Yaweze Kufanyiwa Ukarabati Mkubwa.
Bi.Dumba Ametoa Agizo Hilo Wakati Akipokea Misaada ya Vifaa Mbalimbali Iliyotolewa na Kampuni ya MIWATI ya Kibena TANWATT Kwa Ajili ya Ukarabati wa Baadhi ya Majengo ya Shule Hiyo Kutokana na Uchakavu Uliokithiri Shuleni Hapo.
Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Pia Ameziagiza Kamati za Ujenzi , Ikiwemo Kamati ya Shule ya Msingi Kibena Kuhakikisha Zinafanya Ukarabati Mdogo wa Baadhi ya Madarasa ya Shule Hiyo Ili Kuepusha Majanga Yanayoweza Kujitokeza Kutokana na Mvua Zinazoendelea Kunyesha.
Katika Hatua Nyingine Bi. Dumba Amewataka Viongozi wa Mtaa Huo Kuwahamasisha Wazazi na Walezi Ili Waweze Kutambua Kuwa Shule Hiyo ni Mali Yao na Kuondoa Dhana ya Kuwa Shule Hiyo ni Mali ya Serikali Hali Inayosababisha Baadhi ya Wananchi Kukaidi Kuchangia na Kuitunza Shule Hiyo, Na Hapa Bi.Dumba Anaeleza.
Akiongea Wakati Akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Kwaniaba ya Uongozi wa Shule ya Msingi Kibena ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanwatt Kibena Dokta Rajeev Singa Amesema Vifaa Hivyo Vinathamani ya Shilingi Milioni 1.9 Kwa Ajili ya Kusaidia Ukarabati Shuleni Hapo na Kuongeza Kuwa Wataendelea Kusaidia Katika Shughuli Mbalimbali za Kijamii Kwa Mujibu wa Mikata Inavyowataka Wawekezaji Mbalimbali,Kama Anavyoeleza
Awali Katika Taarifa Fupi Ya Shule Hiyo Iliyosomwa na Afisa Mtendaji wa Mitaa ya Kibena Otmary Daniel Mbangala Imeeleza Kuwa Uchakavu wa Shule Hiyo Umetokana na Kuwa Shule Hiyo Imejengwa Muda Mrefu Kwani Hadi Sasa Ina Miaka 58, Kama Anavyoeleza.
Shule ya Msingi Kibena Ilijengwa Mnamo Mwaka 1956 na Kuanza Rasmi Mwaka 1964 Baada ya Kuzinduliwa na Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere na Hivyo Hali Hiyo Imesababisha Kuwepo Kwa Kiwango Kikubwa cha Uchakavu wa Madarasa Yanayohitaji Ukarabati Mkubwa.
No comments:
Post a Comment