Thursday, March 13, 2014
BAADHI YA WATUMISHI WA MUNGU WADAIWA KUWALAGAI WAATHILIKA WA MAGONJWA SUGU KWAMBA WANAPONYA KWA MAOMBI
Watu Waishio Na Virusi Vya Ukimwi Katika Mkoa Wa Njombe Wamewatuhumu Baadhi Ya
Viongozi Wa Madhehebu Ya Dini Kupotosha Umma Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa
Maombi.
Wakizungumza Mbele Ya Mwenyekiti Mtendaji Wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Tacaids
Fatma Mrisho Baadhi Ya Watu Waishio Na VVU Wamesema Viongozi Wa Dini Wamekuwa
Wakiwalagai Waathirika Wa Ukimwi Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa Maombi Na Hivyo
Kuacha Kutumia Dawa Na Kupunguza Makali (ARV).
Wamesema Hali Hiyo Imesababisha Baadhi Ya Waathirika Kuacha Kutumia Dawa Na
Kwenda Kliniki Na Hivyo Kujikuta Katika Hatari Ya Kushambuliwa Zaidi Na Magonjwa
Nyemelezi Ya Ukimwi Na Hivyo Kuhatarisha Maisha Yao.
Wakiwa Kwenye Kikao Cha Wadau Mbalimbali Wa Ukimwi Wakiwemo Wataalamu Wa
Afya Katika Ukumbi Wa Halmashauriya Wilaya Ya Njombe Baadhi Ya Waathirika Hao
Wamesema Viongozi Hao Wa Dini Wamekuwa Wakichangia Watu Kuacha Kutumia
Dawa Kwa Kuwadanganya Watu Kuwa Wanaponya Ukimwi Kwa Maombi,Na Hapa
Wanaeleza.
Katika Hatua Nyingine Imegundulika Kuwa Baadhi Ya Waathirika Wamekuwa Wakiacha
Kutumia Dawa Hizo Na Badala Yake Wanajiingiza Kwenye Matumizi Ya Pombe.
Peter Mwamasika Ni Askofu Mstaafu Wa Kanisa La Kiinjili La Kilutheri Tanzania Dayosisi
Ya Dodoma Na Kamishina Wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Taifa Kwa Niaba Ya Wakristo
Ambaye Amesema Kuwa Pamoja Na Viongozi Wa Dini Kupinga Matumizi Ya Kondomu
Lakini Wanapaswa Kuwaelimisha Wananchi Njia Sahihi Za Kutokomeza Janga La
Ukimwi.
Tume Hiyo ya Kudhibiti Ukimwi Imeanza Ziara ya Kuwatembelea Wananchi Mjini
Njombe Kwa Siku Mbili Ambapo Pamoja na Mambo Mengine Imewafikia Walimu na
Wanafunzi Kwenye Shule za Msingi Mpechi na Mount Living Stone Ambapo Hapo Kesho
Inahitimisha Ziara Hiyo Ya Siku Mbili Kwa Kutembelea Shule za Sekondari Ili Kubaini
Chanzo cha Maambukizi Hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment