Tuesday, March 11, 2014
JESHI LA POLISI LIMETHIBITISHA KIFO CHA MTUMISHI MMOJA WA MUNGU NA WAWILI KUJERUHIWA KWA AJALI NJOMBE
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE FULGENCE NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE.
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia dereva mmoja Bwana Sadick Twaha kwa
tuhuma za kusababisha kifo cha sister Cloudia Ngailo mkazi wa parokia ya Madunda
wilayani Ludewa baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T 524 CRV yenye tera
T 641 mali ya bwana Evarist Freight wa Dar es Salaam iliyokuwa ikiendeshwa na bwana
Sadick Twaha mkazi wa Isaka Kahama.
Akiongea na mtandao huu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence
Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa katika ajali hiyo
imesababisha majeruhi wawili akiwemo padre Francis Mligo ambae alikuwa dereva wa
gari dogo namba T 185 AWP aina ya Landrover Discover mali ya Kanisa Katholiki
Njombe.
Aidha Kamanda Ngonyani amesema kuwa majeruhi mwingine ni Sister Eitropia Mgani
mkazi wa parokia ya Ihanga ambae hali yake siyo nzuri ikiwa majeruhi wote wamelazwa
nkatika hospitali ya Kibena kwa matibabu zaidi.
Kamanda huyo amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo machi 10 mwaka huu majira
ya saa moja na dakika 40 asubuhi katika kijiji cha Limage kata ya Yakobi Wilayani Njombe
barabara ya Njombe Songea ambapo chanzo cha ajali hiyo bado kinaendelea
kuchunguzwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment