Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, March 19, 2014

MADEREVA DARADARA WAZIKATAA TAX NA BAJAJI NJOMBE





Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe RTO  James Kiteleki Akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Daladala na Taxi Mjini Njombe Mapema Leo Ofisini Kwake

Afisa wa SUMATRA Mkoa wa Njombe Bi. Mery Menard Akizungumza Kwenye Kikao Hicho leo
Mwenyekiti wa Daladala Mkoa wa Njombe Bwana Seleman Mwenda Akitolea Ufafanuzi wa Kero Wanazo zipata Toka Kwa Madereva wa Taxi za Kusalaliza na Bajaji Mjini Njombe

Afande Malwa Akizungumzia Usumbufu Uliopo Mkoani Njombe Katika Masuala ya Usalama Barabarani

Hawa ni Baadhi ya Viongozi wa Daladala na TAXI Mjini Njombe Wakiwa Kwenye Kikao na RTO Njombe.



Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Kitengo cha Usalama Barabarani Kwa Kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu SUMATRA Imepiga Marufuku Utumiaji wa Magari Ambayo Hayajasajiliwa Kwa Ajili ya Kufanya Shughuli za Usafirishaji Abiria.

Akizungumza Kwenye Mkutano na Viongozi wa Vituo Vya Madereva Pikipiki (Bodaboda), Dalaadala na Taxi Kamanda Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe SP James Kiteleki  Amewaagiza Viongozi Hao Kupeleka Majina ya Madereva Wanaofanya Shughuli za Usafirishaji Abiria Bila Kusajiliwa na Wanaosalaliza.

Akijibu Maswali ya Viongozi Hao wa Pikipiki (Bodaboda), Dalaadala na Taxi Ameahidi Kuwachukulie Hatua za Kisheria Madereva Wote Watakaovunja Utaratibu Uliowekwa Huku Akiwataka Wamiliki na Madereva wa Vyombo Vya Moto Kufuata Sheri za Usalama Barabarani na Watu Wengi Wanaotumia Barabara Hizo.

Naye Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Makoa wa Njombe Bi .Mary Menard Amesema Kwa Sasa SUMATRA Kwa Kushirikiana na  Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wanaanza Kutekeleza Agizo Hilo na Kuyakamata Magari Yote Yanayofanya Kazi za Usafirishaji Abiri Yakiwa na Plate Namba za Njano Badala ya Plate Namba Nyeupe.

Awali Wakitoa Hoja na Mapendekezo Yao Kwenye Mkutano Huo Viongozi wa Vituo Vya Madereva Pikipiki (Bodaboda), Dalaadala na Taxi Waliomba Kusogezwa Mbele Kwa Utekelezaji wa Agizo Hilo , Huku Baadhi Yao Wakwalaumu Madeleva Taxi Ambao  Wamekuwa Wakisalaliza na Kusababisha Abiria Kutokaa Kwenye Vituo  Maalumu Vya Kupakia Abiria

No comments:

Post a Comment