MGENI RASMI AKIWASILI KATIKA UKUMBI WA TURBO HII LEO AKIWA NA VIONGOZI WENGINE AKIWEMO MWENYEKITI WA NJORECU PAMOJA NA MENEJA WA NSSF MKOA WA NJOMBE GODWIN MWAKALUKWA WAKIWASILI KATIKA UKUMBI WA MKUTANO
WA UPANDE WA KULIA NI MRAJIS WA VYAMA VYA USHIRIKA NA WA UPANDE WA KULIA NI MKUU WA OPERATION KUTOKA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII NGUSSA SOMOLO
MENEJA WA SHIRIKA LA HIFADHI YA JAMII MKOA WA NJOMBE GODWIN MWAKALUKWA AKITOA UTANGULIZI WA SEMINA ILIYOFANYIKA LEO KATIKA UKUMBI WA TURBO
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIONGEA NA VIONGOZI WA VYAMA HIVYO VYA USHIRIKA
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKITOA HOTUBA
MAAFISA USHIRIKA NA WENYEVITI WA VYAMA VYA USHIRIKA WA KUTOKA WILAYA MBALIMBALI ZA MKOA WA NJOMBE WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA HOTUBA YA MGENI RASMI
PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUMALIZIKA KWA HOTUBA YA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoani Njombe Hii Leo Limetoa Mafunzo Kwa Wenyeviti na Maafisa Ushirika Kutoka Wilaya za Mkoa wa Njombe Jinsi ya Kutoa Mikopo Kwa Vyama Vya Ushirika na Namna ya Wanachama wa Vyama Hivyo Wanaweza Kukopa.
Aidha NSSF Pia Imewataka Wenyeviti na Maafisa Kutoa Elimu na Kuwahamasisha Wananchi Kujiunga na Vyama Hivyo Pamoja na Shirika Hilo la Taifa la Hifadhi ya Jamii na Kuondokana na Dhana yaKuwa SHirika Hilo Lipo Kwa Ajili ya Watu Walioajiriwa Serikalini na Sekta Binafsi.
Awali Akimkaribisha Mgeni Rasmi Kwenye Mafunzo Hayo Meneja wa NSSF Mkoani Njombe Godwin Mwakalukwa Amewakumbusha Waajiri Kupeleka Michango ya Wafanyakazi Wao Kila Mwisho wa Mwezi, Huku Akiwashauri Wananchi Kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Ili Waweze Kunufaika Wakati wa Uzeeni, Huku Akielezea Lengo la Semina Hiyo.
Ngusa Somolo ni Mkuu wa Operation kutoka shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii mkoa wa Njombe ambae amesema kuwa walitegemea kuwa na washiri zaidi ya mia moja na kumi na mbili katika semina hiyo ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Turbo.
Akiongea Wakati wa Kufungua Semina Hiyo Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi amesema Viongozi wa Vyama Vya Ushirika wanatakiwa Kuhakikisha Wanawajibika Kikamilifu Katika Kuwaelimisha Wananchi na Kujiunga na Kuvisimamia Vyama Vyao na Kwamba Wanachama Wake Wanufaike Kama Serikali Inavyokusudia.
Bi Dumba amesema kuwa viongozi wa shirika la hifadhi ya jamii na viongozi wengine wa vyama vya ushirika wanatakiwa kuwafikia wakulima na wananchi ili kutoa elimu juu ya kujiunga na vyama hivyo pamoja na shirika la hifadhi ya jamii na kwamba hali hiyo itasaidia kuwaondoa na hali ngumu wanayoipata kwa sasa.
Kwa Upande Wao Washiriki wa Semina Hiyo Wameipongeza NSSF na Kusema Kuwa Watayafanyia Kazi Mafunzo Waliyoyapata Kwa Kutoa Elimu Kwa Wanachama wa Vyama Vyao na Kuwashawishi Kujiunga na Vyama Vya Ushirika AMCOS.
No comments:
Post a Comment