Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limetolea Ufafanuzi Kuhusu Malalamiko Yanayotolewa na Baadhi ya Wananchi Waliyohoji Uhalali wa Jeshi Hilo Kuwakamata na Kufanya Doria Kwenye Maeneo Mbalimbali ya Vijiji na Mitaa Bila Kutoa Taarifa Kwa Viongozi wa Maeneo Husika.
Akitolea Ufafanuzi Huo Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe SSP Focus Malengo Amesema Kuwa Sheria Haiwalazimishi Askari wa Jeshi la Polisi Kutoa Taarifa Kwa Kiongozi Yoyote wa Kijiji Au Mitaa Pindi Jeshi Hilo Linapotaka Kufanya Uchunguzi Ama Upelelezi wa Kesi Mbalimbali Kutokana na Sababu za Kiintelijensia.
Kamanda Malengo Amesema Licha ya Kuwa ni Muhimu Kutoa Taarifa Kwa Viongozi Hao Lakini Wakati Mwingine Viongozi Hao Husababisha Kuvurugika Kwa Upelelezi Husika.
Pamoja na Hali Hiyo na Baadhi ya Tuhuma Zinazoelekezwa Kwa Jeshi Hilo SSP Malengo Ameseam Jeshi la Polisi Litaendelea Kufanya Kazi Kwa Ukaribu na Jamii Kutokana na Kuendeleza Dhana ya Polisi Jamii Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Njombe.
Hivi Karibuni Wananchi wa Kijiji cha Kinenulo Wilayani Wanging'ombe Wakilalamikia Kitendo cha Askari Polisi Kufikia Kijijini Humo Bila Taarifa na Kisha Kuanza Kuwakamata Baadhi ya Wananchi na Vyombo Vya Moto Zikiwemo Pikipiki.
Aidha Wananchi Hao Walisema Hali Ambayo Inaleta Hofu Kwa Baadhi ya Wananchi na Kuongeza Wasiwasi na Kuendeleza Dhana ya Wananchi ya Kuliogopa Jeshi la Polisi na Kusababisha Kutotoa Ushirikiano Pindi Matukio Yanapojitokeza.
No comments:
Post a Comment