KATIBU WA CHADEMA TAWI LA LUSISI BWANA GODLUCK LEVI
MWENYEKITI CHADEMA TAWI LA LUSISI PIUS MICHAEL NGENDWA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema tawi la Lusisi Wilayani Wanging'ombe kimesema kinatarajia kuanza zoezi la kuwatembelea wananchi ili kubaini changamoto zinazowakabili pamoja na kuwahimiza viongozi wa vijiji na kata kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Akizungumza na Uplands fm Mwenyekiti wa Chadema tawi la Lusisi bwana Pius Michael Ngendwa amesema kuwa chama hicho hivi karibuni kimefanikiwa kufungua tawi la chama hicho ili kupeleka msukumo mkubwa wa maendeleo kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kuwatembelea wananchi kusikiliza kero zao licha yakuwa walichaguliwa ili kuwatumikia wananchi.
Aidha bwana Ngendwa amesema kuwa kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa miundombinu ya umeme na miundo mbinu ya barabara na maji huku akina mama wakikabiliwa na kukosekana na huduma za matibabu jambo ambalo ni kero kwa akina mama wajawazito kijijini humo.
Kwa upande wake Katibu wa Chadema tawi la Lusisi bwana Godluck Levi amesema kuwa chama hicho kina wanachama zaidi ya mia moja mbapo kinatarajia kuunda kamati ya ufuatiliaji wa maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho huku akisema kuwa wananchi wanasikitishwa kuona huduma za umeme zinashindwa kuwafikia licha ya kuwa njia za umeme zimepita karibu na kijiji hicho.
Siku chache zimepita Mbunge wa Jimbo la Njombe magharibi Gereson Lwenge alitolea ufafanuzi kuhusiana na miundombinu ya umeme kupelekwa katika kijiji hicho kwamba kwa bajeti ya mwaka 2013 na 2014 kijiji hicho hakikuwekwa kwenye bajeti ya kuingiziwa huduma ya umeme na kwamba wananchi wategemee kuingiziwa umeme huo katika bajeti ya mwaka 2014 na 2015 ndipo wataweza kufikishiwa huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment