MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKIJIANDAA KUPANDA MTI KATIKA ENEO AMBALO MAADHIMISHO YA SIKU YA UPANDAJI MITI LIMETEULIWA
MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSATAAFU ASERI MSANGI AKIPANDA MTI
KUNDI LA SANAA LA KIBENA ARTS GROUP LIKITUMBUIZA NA KIBAO CHAO CHA MAZINGIRA
FADHA ANNORD NGOLE AKIOMBA MARA BAADA YA WAGENI KUWASILI UWANJA WA MKUTANO
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI. SARAH DUMBA AKITAMBULISHA UGENI ULIOKUWEPO
KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE AKIWA AKIJITAMBURISHA
MAKATIBU WA CCM WILAYA NA MKOA WA NJOMBE
ZAWADI MBWAMBO
MWENYEKITI WA BODI WIZARA YA MALIASILI
WAKATI HOTUBA IKIENDELEA SIKU YA UPANDAJI WA MITI WANANCHI WALIKUWA WAKIBURUDIKIA NA KINYWAJI CHA POMBE ZA KYENYEJI
KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAIMUNA TARISHI AKIZUNGUMZA
AFISA HABARI WILAYA YA NJOMBE LUKERO MSHAURA AKIWA NA WATUMISHI WENGINE WA HALMASHAURI NA WADAU WENGINE WA MAZINGIRA NA VIONGOZI WA DINI
MSANGI AKITOA HOTUBA YA MAADHIMISHO YA UPANDAJI WA MITI
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE EDWIN MWANZINGA AKIZUNGUMZA
HILI NI ENEO LA CHANZO CHA MTO RUAHA MKUU NA MBELE YAKE KUNA MAJENGO AMBAYO NI KIWANDA CHA KAMPUNI YA TANWAT
Mkuu wa Mkoani Njombe Keptein Mstaafu Aseri Msangi Amewataka Wananchi na Taasisi Mbalimbali Kuendelea Kupanda Miti Kwa Wingi Ambayo ni Rafiki na Vyanzo Vya Maji Ili Kutunza Vyanzo Hivyo Pamoja na Mazingira Ili Kukabiliana na Uharibifu wa Mazingira Unaoanza Kujitokeza.
Akizungumza Kwenye Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Kitaifa Yaliyofanyika Mkoani Njombe Kwaniaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Keptein Mstaafu Msangi Amewapongeza
Wananchi na Taasisi Zilizojishughulisha na Upandaji Miti Kwa Lengo la Kutunza Vyanzo Vya Maji na Mazingira
Aidha Keptein Msangi Amewaagiza Viongozi wa Ngazi za Vijiji na Kata Kuhakikisha Wanasimamia na Kumaliza Matukio ya Moto Kichaa Yanayojitokeza Kwa Wingi Katika Wilaya za Mkoa wa Njombe Nchi Nzima na Hapa Anaeleza
CUE......... MSANGI MOTO
Halikadhalika Mkuu Huyo wa Mkoa Amerejea Kauli Yake ya Kusisitiza Kilimo cha Matunda
Huku Akishauri Shughuli Hizo za Upandaji Miti Ziende Sanjaria na Ufugaji Nyuki Ambapo Ameyataka Makapuni na Taasisi Mbalimbali Kuendeleza Zoezi la Upandaji Miti.
Awali Akisoma Taarifa ya Wizara ya Maliasili na Utali , Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Bi. Maimuna Tarishi Amesema Takwimu Zinaonesha Kuwa Katika Kipindi cha Mwaka 2005 / 2006 Hadi 2012 /2013 Iongezeka Kwa Wastani wa Miti Milioni Mia Moja Sitini na Tano Kwa Mwaka Sawa na Asilimia 65 Ambayo Inaendelea Kukua Hadi Sasa Maeneo Mbalimbali Hapa Nchini, Huku Akielezea Baadhi ya Changamoto.
Aidha bi.Tarishi amesema kuwa tathimini ya kitaalamu inaonesha uharibifu wa miti kwa mwaka ni hekta takribani laki nne ambapo ni sawa na asilimia moja nukta moja ya misitu yote nchini na kwamba uharibifu mkubwa wa misitu unasababishwa na matukio ya moto,kilimo cha kuhamahama,uvunaji kwaajili ya mkaa,kuni na ufugaji wa mifugo ambayo haizingatii utaratibu.
Amesema kuwa uharibifu zaidi unatokana na uvamizi na numegaji wa maeneo ya misitu kwaajili ya matumkizi mengine ya kibinadamu kwa mfano makazi,kupitisha njia za umeme,barabara na uchimbaji wa madini ambapo kwa kuzingatia changamoto za uhifadhi wizara ya maliasili na utalii kupitia wakala wa huduma za misitu Tanzania na wadau wengine inaendelea kuimarisha usimamizi wa misitu ya hifadhi na jitihada zaidi zimefanyika kwa kuhifadhi misitu hamsini na tisa yenye jumla ya hekta laki tatu hamsini na tisa na sitini na tatu.
Hata hivyo katibu huyo amesema kuwa misitu kumi na minane imepandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya mazingira asilia na misitu ya miziro,Rondo na uzungwa escapment ipo katika hatua mbalimbali za kutangazwa ili kuwa misitu ya mazingira asilia.
Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Imefanyika Mkaoani Njombe Eneo la Kibeba Chanzo cha Mto Ruaha Kwa Kupanda Miti Takribani Elfu Moja Huku Kaulimbiu ya Mwaka Huu Ikisema Miti ni Uhai Panda Miti Kwanza Ndipo Ukate Mti .
No comments:
Post a Comment