Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, March 30, 2014

WANANCHI IMALINYI WAMUFUKUZA MTENDAJI WA KIJIJI KWA KUSHINDWA KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI KWA WANANCHI



STAKABADHI HII HAITAMBULIKI NA SERIKALI AMBAYO ALIKUWA AKIITUMIA MTENDAJI WA KIJIJI CHA IMALINYI NA HII NDIYO ILIYOMUONDOA

HII STAKABADHI HALALI YA MICHANGO KWA WANANCHI
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA IMALINYI  BWANA ADAM  CHENGUALA AKITOLEA UFAFANUZI BAADHI YA MALALAMIKO YA WANANCHI WA NKIJIJI HICHO 




DIWANI KATA YA IMALINYI ENOCK KISWAGA AKITOA HOTUBA YAKE  MBELE YA WANANCHI WA KIJIJI CHA IMALINYI

AKITOLEA UFAFANUZI  WA KUSOMA TAARIFA ZA HESABU ZA MAPATO NA MATUMIZI KWA WANANCHI AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA MASAULWA

MTENDAJI WA KIJIJI HICHO ALIYEONDOLEWA KWA NGUVU MITON MGOBASA AKIKANUSHA HOJA NA MALALAMIKO ANAYOTUHUMIWA NAYO

DIWANI WA KATA YA IMALINYI ENOCK KISWAGA KIKEMEA TABIA HIYO KAMA IPO NA VIJIJI VINGINE WAACHE KUTUMIA STAKABADHI9 FEKI WATUMIA STAKABADHI ZA HALMASHAURI YA KIJIJI ILIYOTOKA WILAYA YA WANGING,OMBE

A
MWANANCHI HUYO ANAPELEKA STAKABADHI YA KUGUSHI KWA DIWANI WA KATA MBELE YA MKUTANO HUO


WANANCHI WA KIJIJI CHA IMALINYI WAKIWA KWENYE MKUTANO

Wananchi wa kijiji cha Imalinyi leo wamemufukuza afisa mtendaji wa kijiji hicho kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kutowasomea hesabu za mapato na matumizi kwa zaidi ya mwaka mmoja pamoja na kugushi  stakabadhi za michango na tozo zinazochukuliwa kwa wananchi hao.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara wananchi hao wamesema afisa mtendaji huyo kwa kushirikiana na mwenyekiti wa kijiji hicho wamegeuza ofisi ya kijiji kuwa mahakama ya usuruhishi wa migogoro na kesi mbalimbali kwa kuwatoza faini kuanzia shilingi elfu sabini  hadi laki moja huku akidaiwa kuwapatia stakabadhi feki na michaqngo mingine ikishindwa kutolea kwa stakabadhi hizo.

Akijibu tuhuma hizo afisa mtendaji wa kijiji hicho bwana Milton Mgobasa  amekili kutowasomea wananchi hesabu za mapato na matumizi kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusema kuwa chanzo cha kutosoma taarifa za hesabu hizo kwa wakati ni kwamba alikuwa amekaimsishwa ofisi ya kata pamoja na kuwepo kwa safari za kwenda ziara ya mwenge na misafara ya Rais jambo ambalo wananchi hawakulizika na hoja zake.

Aidha bwana Mgobasa amekili makosa kutumia stakabadhi ambazo si za halmashauri ya kijiji, kuchukulia michango na tozo kwa wananchi huku akishindwa kutoa sababu ya kutumia stakabadhi zisizostahili na kusema kuwa yupo tayari kukubaliana na maamuzi yatakayotolewa na wananchi dhidi yake.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Imalinyi bwana  Enock Kiswaga amesema kuwa kufuatia kubaini kuwepo kwa malalamiko ya nwananchi ya kutosomewa taarifa ya hesabu za mapato na matumizi pamoja na kugeuza ofisi ya kijiji kuwa mahakama ya usuruhishi na kuwatoza faini kinyume cha sheria ameamua kuitisha mkutano huo ili kupatiwa majibu kutoka kwa afisa mtendaji huyo na serikali yote ya kijiji.

Aidha bwana Kiswaga amesema kuwa baada ya kujiridhisha kuwa mtendaji huyo anajihusisha na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na fedha za kijiji ameamua kumkabidhi kwa afisa mtendaji wa kata ambae atamsimamia mtendaji huyo ahakikishe anasoma taarifa za mapato na matumizi ndipo akabidhi ofisi ya kijiji hicho na uchunguzi dhidi yake ukifanyika ili hatua kali za kisheria zichukuliwe.

Akizungumza kwa upande wake kaimu afisa mtendaji wa kata ya Imalinyi ambae ni mratibu elimu wa kata hiyo bwana Eusebio Mtasiwa amesema kuwa majibu ya afisa mtendaji huyo wa kijiji ya kwamba alikaimishwa katika ofisi ya kata siyo ya kweli kwani alikaimishwa kwa muda wa siku mbili na kwamba isingemuzuia kusoma taarifa za mapato na matumizi ya wananchi hao.

Kumekuwa na tabia ya watendaji wa vijiji kushindwa kusoma taarifa ya hesabu za mapato na matumizi  kwa wananchi jambo ambalo limekuwa likisababisha wananchi kuwafukuza katika vijiji vyao ambapo watendaji hao serikali imekuwa ikiwahamishia katika vijiji vingine kuendelea na kazi licha ya kutuhumiwa kuhusika na ubadhilifu huo.



No comments:

Post a Comment