Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, January 27, 2014

WAFUGAJI WA KIJIJI CHA MAWINDI WATARAJIA KUNUFAIKA NA NG'OMBE WA MAZIWA .

 DIWANI WA KATA YA IGIMA RUKELO NYAGAWA AKIWASILISHA HOJA HIYO YA HALMASHAURI KUKABIDHI NG'OMBE WA MAZIWA KATIKA KIJIJI CHA MAWINDI WILAYANI WANGING'OMBE MBELE YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI.


Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Inatarajia Kutoa Mkopo wa Ng'ombe 13 wa Maziwa Wenye Thamani Shilingi Milioni 20 Kwa Wafugaji 13 wa Vikundi Vinavyojishughulisha na Ufugaji Kwa Ajili ya Kujikwamua Kiuchumi.

Aidha Halmashauri Hiyo Imewataka Wafugaji Watakaopatiwa Ng'ombe Hao Kuandaa Mazingira ya Kwa Ajili ya Kufugia Mifungo Hiyo Kwa Kushirikiana na
Wataalam wa  Mifugo.

Akizungumza na Uplands Redio Diwani wa Kata ya Igima Lukelo Nyagawa Amesema Ng'ombe Hao Wanatarajiwa Kukabidhiwa Kwa Wafugaji Hao Mwezi Juni Mwaka Huu Mara Baada ya Kukamilisha Ujenzi wa Mabanda ya Kufugia na Kuongeza Kuwa Kwa Awamu ya Kwanza Watapatiwa Wanakijiji wa Mawindi, Huku Akisisitiza Kuitunza Mifugo Hiyo, Kama Anavyoeleza.

Kwa Upande Wao Wananchi wa Kijiji cha Mawindi Wanaotarajia Kupatiwa Mkopo Huo Wameushukuru Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe na Kusema Kuwa Tayari Wameanza Kuandaa Sehemu Kwa Ajili ya Kufugia Ng'ombe Hao, na Hapa Wanaeleza.

Hata Hivyo Wameseam Kuwa Tayari Wameunda Kikundi cha Wanachama 30 Watakaosimamia Mradi Huo Huku Wakiwaomba Wataalam wa Mifugo Kuwa Tembelea Mara Kwa Mara Ili Kubaini Maendeleo ya Mifugo Hiyo.

No comments:

Post a Comment