HUYU NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE EDWIN MWANZINGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE
Hapa
ni Kituo kikuu cha Mabasi Mjini Njombe Ambacho Kinaendelea Kulalamikiwa
na Madereva na Abiri Wengi Kwa Kuwa na Hali Mbaya Kila Unapofika Msimu
wa Masika.
Halmashauri ya Mji wa Njombe Imerejea Tena Kauli Yake na Kusema Kuwa Kwasasa
Halmashauri Hiyo Iko Kwenye Mchakato wa Kujenga Kituo Kipya cha Kisasa cha Mabasi Eneo la
Mjimwema na Kwamba Tayari Hatua za Awali za Ujenzi wa Kituo Hicho Zimeanza.
Akizungumza na Uplands Redio Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Edwin
Mwanzinga Amesema Kwa Sasa Halmashauri Hiyo Haina Mpango wa Kukarabati Kituo Kikuu
cha Mabasi cha Njombe Mjini Kinachotumika Kwasasa Huku Akiwataka Watumiaji wa Kituo
Hicho Kuwa Wavumilivu.
Bwana Mwanzinga amesema kuwa wasafirishaji na abiria na wafanyabiashara wa eneo la kituo kikuu cha mabasi hicho wategemee kutatuliwa tatizo hilo kuanzia mwezi april mwaka huu na kwamba halmashauri haiwezi kupeleka kifusi sasa hivi kutokana na mvua zinazonyesha zitasababisha kuwepo kwa tope ambalo litazidi kuongeza kero kwa abiria na wasafirishaji wa kituo hicho.
Amesema kuwa kituo kipya kinatarajia kukamilika baada ya muda wa miaka minne kuanzia sasa ambapo fedha za kujengea kituo hicho halmashauri inategemea kupata toka kwa wafadhili ambapo mpaka sasa tayari wamekwisha kutuma fedha kidogo takribani milioni mia sita huku wakiendelea kuwatumia nyingine ili kukamilisha kitu cha kisasa kitakachokuwa na hotel,vituo vya mafuta na miundombinu mingine ikiwemo vyoo vya kudumu.
Uongozi Huo wa Halmashauri Umerejea Kauli Hiyo Kufuatia Maafisa Usafirishaji , Wamiliki na
Madereva wa Magari Yanafanya Shughuli za Usafirshaji Abiria Pamoja na Watu Wanaotumia Kituo
Hicho Kulalamikia Ubovu wa Kituo Hicho Hasa Katika Kipindi Hiki cha Mvua.
Aidha Watumiaji wa Kituo Hicho Wameuomba Uongozi wa Halmashauri Hiyo Kufanya Ukarabati
Wakati Wakijipanga Kujenga Kituo Hicho Kipya cha Kisasa Ili Kuwaondolea Adha Wasafiri na
Watu Wanaoendesha Shughuli za Kiuchumi Katika Kituo Hicho.
Kwa Muda Mrefu Watumiaji wa Kituo Kikuu cha Mabasi Mjini Njombe Wamekuwa Wakiuomba
Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kukifanyia Ukarabati Kituo Hicho Huku Majibu ya
Halmashuri Hiyo Yakiwa ni Yaleyale.
No comments:
Post a Comment