Sunday, January 26, 2014
KATIBU MKUU WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA DR WILLBROAD SLAA AMEHUTUBIA MAELFU YA WAKAZI WA NJOMBE MJINI NA KUMDADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA NJOMBE MJINI
HAPA WILLBROAD SLAA ANAMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA NJOMBE MJINI AGREY MTAMBO MWENYE SUTI NYEUSI
WAANDISHI WA HABARI WA KITUO CHA RADIO UPLANDS FM SHABAN LUPA NA MICHAEL NGILANGWA WAKIRUSHA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA KUPITIA RADIO HIYO.
ULINZI NA USALAMA UMEIMARISHWA KUHAKIKISHA AMANI NA UTULIVU INAPATIKANA
MAKADA WA CHADEMA WAKIWA KWENYE MKUTANO HUO
WANANCHI WA NJOMBE MJINI WAKISHANGIRIA KWA FURAHA NA SHANGWE KUBWA BAADA YA KUPATA HOTUBA ILIYOGUSA MAISHA YAO
VIONGOZI WA CHADEMA TAIFA NA KANDA WAKIWA NA MGOMBEA UDIWANI KATA YA NJOMBE MJINI
WILLBROAD SLAA AKITOA HOTUBA YAKE KWA MAELFU YA WAKAZI WA NJOMBE MJINI
WILLBROAD SLAA BAADA YA KUTELEMKA KWENYE NDEGE SASA AKIELEKEA UWANJA WA MKUTANO HUKU AKIWASALIMU WANANCHI WALIOKWENDA KUMPOKEA.
PICHA NA PROSPAL DAUD MFUGALE.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dokta Willbroad Slaa Amesema Chama Hicho Kitaendelea Kutumia Sehemu ya Fedha Zake Zitokanazo na Ruzuku Kwaajili ya Kuwaelimisha na Kuwapigania Watanzania Ili Kuhakikisha Wanaondokana na Kero Mbalimbali Zinazowakabili Kwasasa Ikiwemo Ukosefu wa Huduma za Msingi Kama Vile Afya na Maji.
Aidha Pamoja na Mambo Mengine Dokta Slaa Ametumia Fursa ya Mkutano Huo Kumnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Njombe Mjini Kwa Tiketi ya CHADEMA na Hivyo Kuwataka Wananchi wa Kata Hiyo Kuhakikisha Wanamchagua Mgombea wa CHADEMA na Kukipa Ushindi Chama Hicho Katika Uchaguzi Huo.
Akizungumza Katika Mkutano Mkubwa wa Hadhara Uliofanyika Katika Viwanja Vya NHC Mjini Njombe Dokta Slaa Amesema Njia Pekee ya Wananchi wa Kata ya Njombe Mjini Kuondokana na Kero ni Kuhakikisha Wanakipa Ushindi Chama Hicho Ambacho Kimeendelea Kuaminiwa na Watanzania
Kwa Upande Wake Mgombea wa Udiwani Kata ya Njombe Mjini Kwa Tiketi ya CHADEMA Bw Agrey Mtambo Amesema Endapo Wananchi Watamchagua Kwenye Uchaguzi Huo Atahakikisha Anaondoa Kero Zote Zinazowakabili Wananchi Ikiwemo Michango Isio ya Lazima na Uboreshaji wa Kituo Kikuu Cha Mabasio Mjini Njombe.
Pamoja na Mkutano Huo Kutumika Kama Sehemu ya Kampeni za Udiwani wa Kata ya Njombe Mjini Pia ni Muendelezo wa Mikutano ya Operesheni Pamoja Daima Inayofanywa na Chama Hicho Katika Mikoa Mbalimbali Hapa Nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment