Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, January 28, 2014

AKINA MAMA WANAOFANYA BIASHARA YA POMBE ZA KYENYEJI KATIKA KILABU CHA TUPENDANE WATABIKA NA KUTOA UCHAFU WA HAJA KUBWA CHOONI KWA KUCHOTA NA NDOO NA KUMWAGA ENEO LINGINE


 HIKI NI CHOO CHA WAFANYABIASHARA WA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI CHA NJOMBE MJINI AMBACHO KINAJAA KILA SIKU NA AKINA MAMA HUCHOTA KWA NDOO ZA RITA KUMI NA KUMWAGA KWENYE SHIMO KUBWA LA HAPO WANAPOTOKEA AKINA MAMA HAO.
 HIKI NI CHOO KIPYA KINACHOJENGWA LAKINI KWA SASA KIMESIMAMA KUTOKANA NA SABABU AMBAZO HAZIKUFAHAMIKA.



 HILI NI DAMBO AMBALO LIPO USONI MWA KILABU CHA WAFANYABIASHARA HAO


 HAYA NI MAENEO YA KILABU CHA POMBE ZA KYENYEJI CHA NJOMBE MJINI KINACHOMILIKIWA NA SERIKALI.

Wafanyabiashara wa Vyakula na Pombe za Kienyeji Katika Kilabu cha Tupendane Mjini Njombe Wako Hatarini Kukumbwa na Magonjwa ya Mlipuko Kutokana na Ubovu wa Huduma ya Choo Katika Kilabu Hicho.

Wakizungumza na Uplands Redio Baadhi ya Wafanyabiashara wa Eneo Hilo Wamesema Kuwa Kwa Muda Mrefu Wamekuwa Wakikabiliwa na Tatizo la Choo Kutokana na Choo cha Kilabu Hicho Kujaa Mara Kwa Mara.

Nao Baadhi ya Wananchi Wanaoishi Jirani na Kilabu Hicho Wameuomba Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuhakikisha Kilabu Hicho Kina Kuwa na Huduma Bora ya Choo  Ili Kuepusha Magonjwa ya Mlipuko Hasa Katika Kipindi Hiki cha Mvua.

Kwa Upande Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mji wa Njombe Edwin Mwanzinga Amekiri Kuwepo Kwa Tatizo Hilo na Kusema Kuwa Halmashauri Hiyo lli Muweka Mkandarasi Kwa Ajili ya Kujenga Choo cha Kisasa ,na Kwamba Kutokana na Mkandarasi Huyo Kushindwa Kukalisha Ujenzi wa Choo Wanatarajia Kuvunja Mkataba.
Amesema kuwa zoezi la kufuatilia ujenzi wa choo kipya na cha kisasa alipewa diwani wa viti maalumu Jenne Ngenzi na hivyo atakwenda kulifuatilia ili kujua lilifikia wapi ambapo ikiwezekana watalazimika kuondoa mkataba na mkandarasi wa ujenzi huo.

Wafanyabiashara hao wamekuwa wakilazimika kuchota na nndoo za lita kumi kila siku huku mikononi wakiwa wamevaa karatasi za naironi yaani rambo kama njia ya kujikinga na maradhi yanayoweza kujitokeza kutokana na uchafu huo.
Pamoja na mwenyekitri huyo kukili kuwepo kwa uchakavu wa choo hicho kinachotumika kwa sasa amesema kuwa hajatambua kama mkandarasi aliyeshika kontract kama alipewa pesa ya kianzio huku akikili kuwa choo kipya kimesimama kina muda mrefu pasipo taarifa rasmi na hivyo atakwenda kufuatilia kujua tatizo la kusimama ujenzi huo.
Kwa Mujibu wa Wafanyabiashara na Wananchi Wanaoishi Jirani na Kilabu Hicho
Wameeleza Kuwa Tatizo la Ukosefu wa Huduma Bora za Choo Kilabuni Hapo Limekuwepo Kwa Takribani Miaka Bila Kupatiwa Ufumbuzi Wowote.

No comments:

Post a Comment