KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limeelezea mafanikio yake katika kutokomeza uharifu subu ambapo pamoja na mambo mengine limefanikiwa kuwakamata waharifu na kuwafikisha mahakama ya wilaya ya Njombe na kusomewa hukumu ya kwenda jela kifungo cha miaka 30.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na jeshi hilo kukamilisha taratibu zake za upelelezi na hatimae kuwafikisha katika mahakama ya Wilaya ya Njombe ambapo mnamo january 23 mwaka huu mkazi mmoja wa kijiji cha Mungate alisomewa hukumu ya kwenda jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kuhusika na tukio la ubakaji .
Katika hatua nyingine Kamanda Ngonyani amesema kuwa jeshi hilo pia lilifanikiwa kukamilisha uchunguzi juu ya tukio la mkazi mmoja wa mafinga msikitini Stanley Kaduma 32 pamoja na Shem Mligiliche 22 mkazi wa kijiji cha Ilunda Wilayani Njombe nakupelekwa katika mahakama ya wilaya hiyo na kusomewa hukumu ya kifungo cha kwenda jela miaka 30 na Hakimu Mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya Wilaya ya Njombe Augustino Rwezile mnamo january 23 mwaka huu.
Aidha Kamanda Ngonyani amesema kuwa watuhumiwa hao wote wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha ambapo mnamo octomnber 3 mwaka 2012 walivamia kituo cha kulelea watoto yatima cha ILUNDA ORPHAN CENTER na kuiba fedha na mali mbalimbali ikiwemo digital kamera,simu mbili aina ya sumgsung vyenye jumla ya thamani ya shilingi milioni tisa laki moja na 35 elfu mali ya kituo hicho cha watoto yatima.
Sanjali na hayo kamanda Ngonyani amesema tukio lingine mkazi mmoja wa kata ya mjimwema kijiji cha kahawa Makambako wilayani Njombe Ayubu Palama alitoa taarifa ya kuokota silaha aina ya short gun iliyotengenezwa kwa kienyeji ikitumia risasi za short gun ikiwa imefichwa kichakani wakati mkazi huyo akikata nyasi za kulishia ng'ombe.
Amesema kuwa uchunguzi ili nkubaini wanaoendelea kumiliki silaha kinyume na sheria unaendelea ili kutokomeza uharifu mkoani Njombe
No comments:
Post a Comment