Wednesday, January 29, 2014
WATU SITA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUVUNJA NA KUIBA NA KUJERUHI KWA NJIA YA LUNGU NA NONDO NA KUIBA MALI MBALIMBALI NJOMBE
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE LEO.
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linawashikiliwa watu sita kwa tuhuma za kuhusika na kuvunja
store iliyoko mtaa wa masasi na kuiba mali mbalimbali za mfanyabiashara Merick Vintan Mgina
mkazi wa mtaa wa Mgendela kata ya Njombe mjini zenye thamani ya shilingi milioni nane mali ya
Merick Vintan Mgina pamoja na tukio la pili la wizi wa shilingi milioni sita na elfu themanini mali ya Benki ya NBC ya Njombe mjini.
Akizungumza na mtandao huu www.michaelngilangwa.blogspot.com kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence
Ngonyani amesema kuwa kufuatia tukio hilo jeshi la polisi liliendesha msako mkali na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa watano Joseph Sanga mkazi wa kibena,Wito James Mlowe mkazi wa
mwenmbetogwa mkoani Iringa,Rajabu Makweta,Michael Kilumile na Geoge Kilumile wakazi wa
mjini Njombe.
Aidha kamanda Ngonyani amesema katika msako uliofanyika januari 27 mwaka huu watuhumiwa
Geoge Kilumile na Michael Kilumile walikamatwa wakiwa na mali za wizi walizoiba mnamo
januari 26 mwaka huu majira ya saa saba usiku katika mtaa wa masasi kwenye store ya
mfanyabiashara Merick Vintan Mgina ambazo ni konyagi box 11,red bull katoni 10 huku mali
nyingine zikiendelea kutafutwa.
Kamanda Ngonyani amesema kuwa katika msako huo pia walifanikiwa kumkamata mkazi mmoja
wa mtaa wa Matalawe Jackson Simkoko baada ya kukutwa na fedha zilizoibiwa katika ghala la
mbolea la kampuni ya Primium lililoko maeneo ya Banki ya NBC mjini Njombe .
Katika tukio lingine kamanda Ngonyani amesema watu wawili Hezron Fate na Stela Lugona
wamejeruhiwa na kuporwa mali mbalimbali na fedha shilingi milini moja na laki tatu na watu
wasiyofahamika baada ya kuvunja nyumba yao ambapo jumla ya thamani ya vitu na fedha ni
shilingi milioni mbili na laki mbili ziliporwa na watu hao na kuwajeruhi kwa kutumia lungu na
nondo na kwamba hakuna mtuhumiwa anaeshikiliwa na jeshi hilo.
Amesema kuwa tukio lingine mkazi mmoja wa kijiji cha Itipingi kata ya Mahongole Albano
Kilumile 16 alifariki dunia baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na
upepo iliyonyesha mnamo january 27 na kusababisha kifo hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment