Wananchi wa mtaa wa kambalage eneo la block x wakiwa kwenye mkutano wa hadhara mtaani humo wakitoa maoni juu ya ujenzi wa soko la biashara na vibanda.
Afisa biashara halmashauri ya mji Edward Mdenu akijibu maswali ya wananchi wa mtaa wa block x.
Mzee akitaka kupunguziwa asilimia za kulipia mapato na kuongezewa muda wa ujenzi wa vibanda na matazamio ya biashara mtaani humo.
Viongozi wa halmashauri ya mji akiwa pamoja na mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa katikati mezani.
Diwani wa kata ya Uwemba Mwalongo akitoa ufafanuzi zaidi juu ya biashara na gharama zake.picha na Michael Ngilangwa.
Wananchi wa Eneo la Block X Mtaa wa Kambarage Hapo Jana Wameshindwa Kuafikaana na Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Juu ya Ulipaji Kodi Mara Baada ya Kukamilika Kwa Ujenzi wa Vibanda Vya Soko la Mtaa Huo.
Wananchi Hao Wameshindwa Kufikia Muafaka na Uongozi Huo wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kwa Madai Kuwa Muda Waliopewa wa Miezi Sita Kwa Ajili ya Kujenga Vibanda Hivyo ni Mchache , Ambapo Wamependekeza Kuongezewa Muda wa Miaka Mitatu wa Ujenzi na Matazamio ya Biashara Pamoja na Kupunguziwa Asilimia Kumi ya Ulipaji wa Mapato na Kulipa Kati ya Asilimia Tatu na Nne ya Mapato
Wakiongea Kwenye Mkutano Huo Wananchi Hao Wamesema Kuwa Kutokana na Kiwango Kikubwa cha Ulipiaji Mapato na Muda wa Matazamio ya Biashara Kuwa Mchache Inapelekea Wafanyabiashara Kutoyatumia Masoko Hayo Huku Wakitolea Mfano Soko la Mtaa wa Joshoni.
Kufuatia Maombi ya Wananchi wa Mtaa Huo , Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edward Mdemu Kwaniaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ameahidi Kutoa Majibu ya Maombi Yao
Baada ya Miezi Miwili Mara Baada ya Uongozi wa Halmashauri Hiyo Kukutana na Kujadili Maombi Hayo ya Wananchi.
Akiongea Kwenye Mkutano Huo Bwana Mdemu Amesema Wafanyabiashara Wanatakiwa Kukamilisha Ujenzi wa wa Vibanda Hivyo Ndani ya Miezi Sita na Kulipia Mapato Kwa Asilimia Kumi .
Kutokana na Kutoafikiana Kwa Wananchi na Uongozi wa Halmashauri Hiyo Mwenenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Vibanda Vya Soko la Mtaa Huo Bwana Saimon Kengese Ameahirisha Mkutano Huo , Ambapo Unatarajiwa Kufanyika Tena Baada ya Miezi Miwili.
No comments:
Post a Comment