Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, January 12, 2013

NAIBU MEYA AWAASA WANANCHI KUTOHUDHURIA KATIKA MIKUTANO ISIYO NA TIJA KATIKA MAENDELEO YA NCHI

Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki akifungua mdahalo

Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki ameeleza kuwa binadamu wanachangia kwa asilimia kubwa katika mabadiliko ya tabia ya nchi.
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa mdahalo wa mabadiliko ya tabia ya nchi ambao umeandaliwa na muunganiko wa mashirika yasiyo ya kiserikali ICISO-UMBRELLA katika jimbo la Iringa mjini.
“Binadamu tumechangia kwa wingi katika mabadiliko ya tabia nchi kutokana nay ale ambayo tunayafanya ikiwemo kutolkujiwekea mazoea ya kutunza mazingira pamoja na kupanda miti” alisema Ndaki.
Amewataka wananchi wote waliofika na wanaopewa elimu hii ya mabadiliko ya tabia nchi kutendea kazi na kuhakikisha mazingira yanatunzwa ipaswavyo ili kuepuka mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanachangia maendeleo hasi katika jamiii.
Pia amewataka wananchi kujijengea tabia ya kuhudhuria katika midahalo mbalimbali inayoandaliwa ambayo inahusu maendeleo ya nchi kwa ujumla na  kuondokana na tabia  kuhudhuria katika masuala yasiyo na maana ambayo hayana mchango chanya katika jamii na taifa kwa ujumla.
Katibu wa ICISO Raphaeli Mtitu akioa maelezo kuhusu lengo la mdahalo kulia ni mmiliki wa mtandao huu akirusha mdahalo huo live katika redio Overcomers fm.

Naye Katibu wa ICISO katika mkoa wa Iringa Raphaeli Mtitu amebainisha kuwa lengo kuu la midahalao hii ni kuwaelimisha wananchi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi hi wote ambao ni huku ikiwahusisha wananchi wote Na pia kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kuhusu mabdailiko ya tabia nchi .Francis Godwin chanzo cha habari hii Iringa.

No comments:

Post a Comment