Saturday, January 12, 2013
MABALOZI NA WENYE VITI WATAKA MALIPO KWA KAZI KUBWA WANAYOIFANYA KWA WANANCHI.
DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI NA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE MH.LUPYANA FUTE AKITOA UFAFANUZI JUU YA MALIPO YA POSHO KWA WENYEVITI NA MABAROZI WA MITAA NA VIJIJI.
Mabalozi na Wenyeviti wa Mitaa Mjini Njombe Wamelalamikia Kitendo Cha Wao Kuendelea Kufanya Kazi Hizo Kwa Muda Mrefu Sasa Bila ya Kuwa na Malipo Rasmi Kutoka Mamlaka Zinazosimmia Serikali za Mitaa.
Aidha Viongozi Hao Wamesema Kuwa Kitendo Cha Wao Kutolipwa Kimekuwa Kikiwashawishi Baadhi ya Wenyeviti na Mabalozi Kujihusisha na Vitendo Vya Rushwa na Hivyo Kusababisha Kukiuka Maadili ya Uongozi.
Wakizungumza Wakati wa Kuhitimishwa Kwa Ziara ya Siku Nne ya Diwani wa Kata ya Njombe Mjini ya Kutembelea Mitaa ya Kata Hiyo,Wenyeviti na Mabalozi Hao Wamesema Kuwa Pamoja na Kutekeleza Majukumu Yao Kikamilifu Ikiwemo Ukusanyaji wa Michango na Ulinzi wa Amani Lakini Bado Wamekuwa Hawana Malipo Rasmi Hivyo Kuomba Serikali kuwafikiria Juu ya Suala Hilo.
Akizungumzia Hali Hiyo Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Bw Lupyana Fute Amesema Malalamiko ya Viongozi Hao ni Changamoto Kwa Chama Cha Mapinduzi CCM Kuhakikisha Kinaongeza Mapato Yake ya Ndani Ili Kuweza Kuwalipa Viongozi Hao Kwa Kuwa Pia Wamekuwa Wakisimama Kama Viongozi wa Chama Kwenye Mitaa Yao.
Kumekuwa na Mjadala Kuhusu Malipo ya Viongozi wa Mitaa na Wenyeviti wa Vijiji Ambao Kwa Muda Mrefu Sasa Wamekuwa Wakitaka Kutambulika Rasmi Katika Malipo Kulingana na Majukumu Yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment