Friday, January 11, 2013
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASSERI MSANGI AMEZINDUA LEO BODI YA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI MAZINGIRA
Wafanyakazi wa mamlaka ya maji mjini Njombe wakiwa ukumbini wakimsubiri mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Assery Msangi Ameitaka Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Njombe NJUWASA Kusimamia Kwa Karibu Mapato na Matumizi ya Mamlaka Hiyo Kama Njia Mojawapo ya Kuboresha Huduma ya Maji Mjini Njombe.
Aidha Mkuu Huyo wa Mkoa Pia Ameitaka Bodi Hiyo Kuweka Mikakati Thabiti ya Utunzaji wa Mazingira na Vyanzo Vya Maji,Kuwafungia Wateja Dira za Maji Kwa Asilimia Mia Moja Pamoja na Kukusanya Madeni Yote ya Maji Ikiwemo Usimamizi wa Miradi Yote ya Maji Inayotekelezwa Kupitia Program ya Maendeleo ya Sekta ya Maji.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba akitoa hotuba kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe katika uzinduzi wa bodi mpya ya mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mjini Njombe.
Akizungumza Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Maji Mjini Njombe NJUWASA,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Amesema Bodi Hiyo Inapaswa Kusimamia Utekelezaji wa Mipango Yake Kwa Kuwa Bado Huduma ya Maji Katika Mji wa Njombe Imekuwa Sio ya Kuridhisha
Wajumbe na wadau wa maji wakipokea hotuba ya mgeni rasmi kwa makini ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe.
Edwini kilasi ni katibu wa kamati ya uhamasishaji maji toka chanzo cha mto nyenga magoda akihamasisha utunzaji vyanzo vya maji ili kuwa na uhakika wa kupata maji na kukemea uchomaji moto hovyo.
Awali Akisoma Taarifa ya Hali ya Huduma ya Maji Mjini Njombe Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Njombe Bw Daud Majani Amesema Tatizo la Maji Katika Mji wa Njombe Linatokana na Upungufu wa Maji Katika Vyanzo Wakati wa Kiangazi
Mkurugenze mamlaka ya maji safi na taka Njombe mjini Daud Majani akisoma taarifa ya utekelezaji wa maji ukumbi mdogo wa halmashauri ya mji Njombe kwa mgeni rasmi.
Amesema Mfumo wa Maji Katika Mji wa Njombe ni wa Zamani Uliojengwa Katika Miaka ya 1982 Ambao Kwa Sasa Umezeeka na Kusababisha Kupasuka Kwa Mabomba Mara Kwa Mara Hali Inayosababisha Upotevu wa Maji na Gharama Kubwa za Matengenezo
Kutokana na Hali Hiyo Mamlaka Inalazimika Kuweka Wazi Mipango Yake ya Muda Mfupi na Ile ya Muda Mrefu Itakayosaidia Kupunguza na Kumaliza Kabisa Tatizo la Maji Mjini Njombe.
Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Njombe OCD Lucy Mwakafulila akiwakilishwa na mkuu wa kituo cha polisi Njombe mjini Andrew Mchome .
Kwa Sasa Mji wa Njombe Unapata Maji Kutoka Vyanzo Vya Magoda,Wikichi na Lunyanyu Vikiwa na Uwezo wa Kuzalisha Wastani wa Zaidi ya Lita Millioni Tatu Kwa Siku Ikilinganishwa na Mahitaji Halisi ya Zaidi ya Lita Millioni Nane Kwa Siku.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji safi na mazingira mjini Njombe Alphonce Mkongwa ameishukuru wizara ya maji na kuahidi kushirikiana na viongozi wengine ili kufanikisha kufikisha huduma ya maji mjini hapa.
Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji na mazingira Njombe mjini akitoa neno baada ya uzinduzi wa bodi hiyo. picha na Michael Ngilangwa.
Bodi ya mamlaka ya maji safi na mazingira mjini Njombe inaundwa na wajumbe kumi ambao miongoni mwao akiwemo katibu tawala wa mkoa wa Njombe bi.Mgeni Buruani,mkurugenzi halmashauri ya mji George Mkindo na viongozi wawakilishi wengine wanaounda safu ya wajumbe kumi akiwemo mwakilishi wa madiwani wote wa halmashauri ya mji wa Njombe Edwini Mwalongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment