Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, January 3, 2013

SHUGHURI ZA UGONGAJI KOKOTO ZINAENDELEA TANGU TUPATE UHURU ENEO LA KWALE MTAA WA KAMBALAGE NJOMBE




 Haya ni mawe ambayo yaligunduliwa na mababu zetu enzi za ukoloni  huko mtaa wa Kambalage.

Serikali ya Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe Imewataka Wafanyabiashara Wa Mawe wa Eneo la Kambarage Kutunza Mazingira Kwa Kujihepusha na Vitendo Vya Ukataji Miti Wakati wa Uendeshaji wa Kazi Hizo.

Mmmoja wa wananchi wanaohusika na ugongaji kokoto aina ya zege akiwa kazini.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage Bw Pankras Matinya Amesema Pia Wafanyabiashara Hao ni Vema Wajihadhari Dhidi ya Ajali Zinazoweza Kujitokeza Kutokana na Maeneo Wanayofanyika Kazi Kuwa Katika Eneo Linalozungukwa na Mawe Mengi.

 Mgongaji kokoto na mawe akiwa ndani ya shimo kubwa la mawe akiendeleza shughuli za ugongaji mawe.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa mitaa ya Kambalage na Idundilanga Telesina Manga Amesema Kupitia Mradi Huo Zaidi ya Wakazi Mia Moja Wamefanikiwa Kupata Ajira na Hivyo Kupunguza Tatizo la Uhalifu Mitaani.


 Miamba ya mawe imetajwa kuongeza ajira  kwa wakazi wa kambalage licha ya zana duni zinazotumika.


Pamoja na wakazi hawa kujipatia ajira lakini je utunzaji mazingira ukoje?

 Shughuli za kazi za endelea akina baba kwa akina mamana watoto wao chakula kimechukuliwa kazini hadi jua lizame.
 Mashine hizi zilisahaulika baada ya kumaliza haja ya kutengeneza barabara kwa kiwango cha rami Njombe Songea bado zipo katika mtaa huo.


Kwa Upande Wao Baadhi ya Wafanyabiashara Hao wa Kokoto Wamesema Miongoni Mwa Changamoto Zinazowakabili ni Pamoja na Ukosefu wa Vifaa Kwa Ajili ya Kufanyia Kazi Zao




Hii ni mitambo ya mashine za kutengeneza kokoto iliyotumiwa na wazee wa zamani wakati barabara ya Njombe songea ikiwekwa rami .

No comments:

Post a Comment