Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, January 6, 2013

HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE INATARAJIA KUKABIDHI NG'OMBE 15 KWA KIKUNDI CHA TUWEZESHANE MFEREKE.

Afisa mtendaji kata utaringoro mwenye koti jeusi ambae ni mgeni rasmi akiwa na viongozi wa kijiji cha mfereke.

Halmashauri ya Mji wa Njombe Inatarajia Kukabidhi Mifugo Kwa Wakazi wa Kijiji Cha Mfereke Kata ya Utalingolo,Wilayani Njombe Kupitia Mradi wa Kopa Ng'ombe Lipa Ng'ombe, Mradi Ambao Umelenga Kuwawezesha Wananchi Hao Kujiongezea Kipato na Kuondokana na Umasikini.

Akizungumza na Wananchi wa Kijiji Cha Mfereke Kwa Niaba ya Diwani wa Kata ya Utalingolo Bw Boniventure Fwalo,Afisa Mtendaji wa Kata ya Utalingolo Bw Stanley Mgohele Amesema Mifugo Hiyo Itakabidhiwa Kwa Watu Kumi na Watano Walio Kwenye Vikundi.

Wananchi mfereke wakitoa hoja namna na kutumia ufugaji wa ng'ombe wa maziwa wa kisasa.

Amesema Mradi Huo ni Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Kwa Kuwawezesha Wananchi Kuendesha Shughuli Zao  za Ufugaji Kwa Njia za Kisasa na Kuifanya Sekta ya Ufugaji Kuwa Yenye Tija.

Afisa mtendaji wa kijiji cha mfereke akitoa muongozo wa uchaguzi wa viongozi wa kikundi  kijijini humo.

Katika Mkutano Huo Pia Walichaguliwa Viongozi Watakaosimamia Shughuli Mbalimbali za Ufugaji Zitakazosimamiwa na Kikundi cha TUWEZESHANE MFEREKE,KOPA NG'OMBE,LIPA NG'OMBE Ambapo Bw Arloyce Ngole amechaguliwa kuwa mwenyekiti Wakati Stanley Mgohele akichaguliwa kuwa katibu.

Mwenyekiti kikundi  cha tuwezeshane mfereke kopa ng'ombe lipa ng'ombe .

Akizungumza Mara Baada ya Uchaguzi Huo Afisa Mifugo Kata ya Utalingolo Bw Keneth Karinga Amesema Viongozi Hao Waliochaguliwa Wanapaswa Kusimamia Baadhi ya Changamotro Zinazowakabili Wafugaji Ikiwemo Lishe ya Mifugo Hiyo na Makazi Salama.
 Hapo chini ni Afisa mifugo kata utaringoro Keneth Kalinga.

No comments:

Post a Comment