Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, January 7, 2013

MKAZI MMOJA WA KIJIJI CHA MFARASI WILAYA YA LUDEWA MKOA WA NJOMBE AUWAWA NA WATU WASIYOFAHAMIKA

 Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani akiwa ofisini kwake.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia  Consolatha Mgimba na Keneth Mkorongo  Wote Wakazi wa Mfarasi Wilayani  Ludewa Kwa  Mahojiano Zaidi Juu ya Tuhuma za Kuhusika na Mauwaji yaliyomkuta  Nikodemu Mwalongo

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Januari Nne Mwaka Huu , na Kuongeza Kuwa Marehemu Nicodem Mwalongo Aliuwawa Kwa Kukatwakwa Sehemu Mbalimbali za Mwili Wake na Kitu Chenye Ncha Kali na Kutenganishwa Kichwa na Kiwiliwili na Kisha Kutupwa Kando ya Mto.

ACP Ngonyani Amesema Mauwaji Hayo Yanahusishwa na Imani Potofu za Kishirikina Ambapo Amewataka Wananchi Kutojichukulia Sheria Mkononi na Kwamba  Jeshi la Polisi Linaendelea na Upelelezi Ili Kubaini Chanzo cha Tukio Hilo.
picha na Michael Ngilangwa.

No comments:

Post a Comment