Kaimu meneja wa shirika la Tanesco wilaya ya Njombe akiwa ofisini kwake.
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Wilayani Njombe Limewahakikishia Wananchi na Wateja Wake Kuendelea Kupata Huduma Bora na Uhakika Licha ya Kupunguzwa Kwa Gharama za Uunganishaji Jambo Linalotia Hofu ya Kuongezeka Kwa Wateja na Kuongezeka Kwa Mahitaji ya Nishati Hiyo.
Aidha Shirika Hilo Pia Limewahakikishia Wateja Wake Wapya Kuunganishiwa Huduma Hiyo Katika Kipindi Kifupi Kisichopungua Siku Thelathini Kupitia Punguzo Jipya Kwa Wale Wasiozidi Umbali wa Mita Thelathini Kutoka Kwenye Jengo Husika.
Kaimu Meneja wa TANESCO Wilaya ya Njombe Bw Omari Amir Ally Amesema Kuanzia Januari Mosi Mwaka Huu TANESCO Ilitangaza Punguzo la Uunganishaji wa Umeme Kwa Wateja Wake Lengo Likiwa ni Kuhakikisha Kila Mtanzania Anapata Huduma Hiyo.
Amesema Kupitia Mpango Huo Wanatarajia Kuongeza Idadi ya Watanzania Wanaopata Huduma ya Umeme Kwa Mwaka 2013 Hadi Kufikia Asilimia 30 Pamoja na Kuongeza Mapato ya Serikali na Shirika Hilo.
Amesema Kwa Kuwa Punguzo Hilo Halihusiani na Matumizi ya Kawaida Kwa Wale Walio na Huduma Hiyo Kwa Sasa,Hivyo ni Vema Wananchi Wakaendelea Kuzingatia Matumizi Sahihi ya Umeme.
Kuhusu Mpango wa Kuwafikishia Wananchi wa Vijijini Huduma Hiyo ya Umeme,Bw Omari Amesema TANESCO Kwa Kushirikiana na Wakala wa Umeme Vijijini REA Wamekuwa Wakishirikiana Kuhakikisha Kila Kijiji Mkoani Njombe Kinapata Huduma ya Umeme
Aidha kaimu meneja huyo amesema kwa mwaka 2013 shirika la umeme Tanzania TANESCO Kwa wilaya ya Njombe linatarajia kuvifikia vijiji zaidi ya 40 kwa kushirikiana na makampuni ya umeme Tanzania ambapo amewaomba wateja wake kujitokeza kwa wingi kuomba kuingiziwa huduma hiyo ambapo itachukua muda wa siku thalathini tangu alipoomba mteja.
No comments:
Post a Comment